Wednesday, November 26, 2014

PICHA, JINSI SITTA ALIVYOWATULIZA WAPINZANI KUHUSU UFISADI WA ESROW,

Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi leo Novemba 26, 2014.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizugumza na Mbunge wa Viti Maalum Rachel Mashishanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urambo, Mh. Samuel Sitta (katikati) akiwatuliza  na baadhi ya wabunge wa Upinzani, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014

Tumeuanza Mwaka wa Watawa Duniani, 2014 - 2016


Makanisa mahalia sehemu mbali mbali za dunia, yataadhimisha Ibada ya Misa na kufanya mikesha ya sala na tafakari kama sehemu ya mchakato wa uzinduzi wa Mwaka wa Watawa Duniani, uliotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko. Waamini wanaalikwa kusali na kumwomba Roho Mtakatifu ili aweze kulikirimia Kanisa neema na baraka ili kujenga na kulipyaisha Kanisa katika maisha na utume wake
Maadhimisho ya Mwaka wa Watawa Duniani yanakwenda sanjari na Jubilee ya miaka 50 tangu Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walipochapisha Waraka kuhusu Fumbo la Kanisa, Lumen Gentium, inayojulikana kama Mwanga wa Mataifa, Kanisa kama Fumbo la Mwili wa Kristo; linaloonekana na lile lisiloonekana; umuhimu wa Taifa la Mungu katika kushiriki katika maisha na utume wa Kanissa pamoja na kukuza ari na moyo wa kimissionari.

Mama Kanisa pia anaadhimisha Jubilee ya miaka 5o tangu Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walipotoa Tamko kuhusiana na Maisha ya Kitawa: Perfect Caritatis, yaani Upendo Mkamilifu, Waraka uliowataka Watawa kupyaisha maisha yao, kwa kutoa nafasi ya kwanza katika maisha ya kiroho, mashauri ya Kiinjili, maisha ya kijumuiya pamoja na malezi makini kwa wale wote wanaotaka kujisadaka kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake.

Haya ni matukio makuu yatakayoliwezesha Kanisa kufanya tafakari ya kina katika maisha na utume wa Watawa sehemu mbali mbali za dunia. Mwaka wa Watawa Duniani unazinduliwa rasmi, Jumamosi jioni tarehe 29 Novemba 2014 kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Makuu, lililoko mjini Roma kwa Ibada na Mkesha wa Sala, kuanzia saa 1:00 Usiku. Tarehe 30 Novemba, 2014, Jumapili ya kwanza ya Kipindi cha Majilio, kutafanyika Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya.

Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume linasema kwamba, matukio haya ni muhimu sana katika uzinduzi wa Mwaka wa Watawa Duniani, kwa kujiweka chini ya ulinzi na usimamizi wa Bikira Maria, Mama wa Mungu na msimamizi wa maisha ya kitawa. Hiki ni kipindi cha matumaini, sala na tafakari ya kina kuhusu matendo makuu ya Mungu katika maisha ya Watawa wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya Mungu na jirani zao, kwa kutambua kwamba, imani ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambayo Watawa wanapenda kuwamegea na kuwashirikisha wengine.

Ninyi Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina Langu......

Nifuraha kwetu Kuona yale tunayofanya yana sifa na Utukufu kwa Mungu, tokea 2011 hadi leo 2014 utume wetu upo na unazidi kuimara, tunawashukuru sana Walezi wetu na Wadau wetu wote kwa michango yao mbali mbali, hapo juu vijana wa wa parokia ya Boko wakiwa na Paroko wa Parokia ya Kigenge Chini Jimbo kuu la Arusha


Askofu Nzigirwa akiongoza Ibada ya Matawi Don Bosco, ikiwa ni siku pia ya Azimisho la Vijana Ulimwenguni ilikuwa mwaka 2012.


Mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rafael, Baada ya Semina ya Siku Moja iliyofanyika katika Kijiji cha Furaha Mbweni mwaka 2011

Baadhi ya Vijana wa Kigango cha Bunju, kwa sasa Parokia ya Bunju wakiburudisha kwenye Sherehe ya Pentekoste ilikuwa mwaka 2012.


















Monday, November 24, 2014

Changamkieni Uinjilishaji wa kina kwa furaha na unyofu wa moyo Ungana nasi tena 2015, Kiabakari - Musoma.


Askofu Beatus Kinyaia wa Jimbo la Mbulu

Beatus Kinyaia ateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.

Hatimaye leo baba Mtakatifu Papa Francisco amempandisha kutoka  askofu hadi kuwa askofu Mkuu askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.


Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor  tarehe 25 juni, 1989.


Aliteuliwa kuwa askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, nakusimikwa/ wekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo  kuwa askofu wa jimbo la Mbulu tarehe 2 Julai 2006.


Leo tarehe 06 Novemba, 2014 ameteuliwa kuwa askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa jimbo kuu.

Atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.

Tuesday, November 18, 2014

Ni kwanini vijana wanaogopa ndoa (kwanini vijana hawataki kuanzisha kanisa dogo)

kuelekea kwenye semina ya Mwaka wa familia tarehe 28-29/11/2014. vijana wanaandaliwa kujenga familia Bora familia ya Kikristo, familia ambayo ni kanisa Dogo, kanisa la nyumbani
 
Matunda ya familia bora ni kuwa na Imani, mapendo na matumaini miongoni kwa wanafamilia, kazi mbayo ni kubwa, familia ilikabiliana na kinzani pamoja na changamoto kubwa za kitamaduni, lakini imani ikaendelea kukua na kuota mizizi katika familia zetu,

tunu za maisingi ya Kikristo kuleta mabadiliko miongoni mwa wa vijana ambao walianza kupata malezi hayo tokea utotoni ,hapo ndipo huibuka miito ya  kipadre na kitawa, neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
 

Kwa sasa vijana  tunaendelea kukabiliana na changamoto mbali mbali katika maisha, hasa kutokana na ongezeko la umaskini, hali ambayo inazifanya familia nyingi kutafuta njia za mkato; mambo ambayo wakati mwingine yanahatarisha imani na matokeo yake ni watu kukata tamaa. Baba Mtakatifu anasema, Familia inapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza kwani ni msingi wa Jamii, mahali ambapo watu wanajifunza kuishi kwa pamoja, licha ya tofauti zao msingi na kwamba ni mahali pa kurithisha imani, dhamana inayotekelezwa na wazazi. Familia ni madhabahu ya Injili ya Uhai, inayopaswa kudumishwa na kuendelezwa.

Wanandoa ambao wengi ni wazazi wetu na vijana wenzetu wadumishe uaminifu na mapendo ya ndoa, wasaidie majiundo ya kina kwa watoto wao sanjari na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia yanayojikita katika Mafundisho tanzu ya Kanisa na kumwilishwa katika uhalisia wa maisha, ili kuwa kivutio kwa vijana wanajianda kuingia kwenye wito huo.

Viongozi wa Kanisa waendelee kuwa karibu zaidi na vijana katika malezi na makuzi yao, ili waweze kuwa na utambulisho makini, tayari kushiriki katika kazi ya uumbaji kwa kujikita katika wito wa ndoa au Daraja takatifu au maisha ya kitawa kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. Vijana wafundwe kuchuchumilia usafi wa moyo pamoja na kukuza ushirikiano miongoni mwa utume wa vijana wa Parokia hizi, ili wote waweze kujisikia kuwa wako ndani ya Familia ambayo kimsingi ni Kanisa dogo la nyumbani.
...bonjeza hapa Kuendelea kusoma hapa


Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki Ifakara

Mwaka wa Imani uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita na kuhitimishwa kwa kishindo kikuu na Papa Francisko, lilikuwa ni tukio la neema kubwa kwa maisha na utume wa Kanisa. Ilikuwa ni nafasi kwa waamini kupitia tena Mafundisho ya Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, ili kuweza kuyapyaisha katika uhalisia wa maisha na utume wa Kanisa katika ulimwengu mamboleo.

Mwaka wa Imani, ulikwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 20 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipochapisha kwa mara ya kwanza Katekesi Mpya ya Kanisa Katoliki, bila kusahau Kitabu cha Sheria za Kanisa; matunda makuu ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Waamini kwa namna ya pekee kabisa walihamasishwa kufanya tafakari ya kina kuhusu Imani wanayoungama katika Fumbo la Utatu Mtakatifu, Kanisa na Mambo ya nyakati.

Waamini walihimizwa kutambua umuhimu wa maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, ili waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kujipatia neema na baraka zinazotolewa na Mama Kanisa. Mwaka wa imani, ulikuwa ni nafasi kwa waamini kujikita katika ushuhuda unaoonesha imani tendaji kwa kukumbatia Amri za Mungu kama dira na mwongozo wa maisha yao ya kiroho na maisha ya hadhara.

Waamini kwa mara nyingine tena, walihimizwa na Mama Kanisa kumwilisha imani yao kwa Kristo na Kanisa lake kwa njia ya Sala na Matendo ya huruma. Kwa maneno machache, Mwaka wa Imani, ilikuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina na mapana kuhusu: Imani, Sakramenti za Kanisa, Amri za Mungu na Maisha ya Sala. Mwaka wa Imani, kimekuwa ni kipindi cha neema ambacho kimeyasaidia Makanisa mahalia kujiwekea mbinu mkakati wa kuimarisha imani kwa njia ya Sinodi za Majimbo au Mwendelezo wa Maadhimosho ya Mwaka wa Imani kwa kuchagua mada mbali mbali kadiri ya mahitaji ya Kanisa mahalia.

Askofu Salutaris Melchior Libena wa Jimbo Katoliki la Ifarakara, Tanzania, katika mahojiano maalum na Gazeti la AMECEA anasema kwamba, mara baada ya kuadhimisha Mwaka wa Imani, kulionekana kwamba, kunahitaji la kuendelea kuwaimarisha waamini katika Mafundisho tanzu ya Kanisa kwa kujikita hasa zaidi katika Katekesi ya kina, zoezi la kiroho linaloigusa Familia ya Mungu Jimboni Ifakara.
http://viwawaboko.blogspot.com/p/mak.htmlKutokana na hitaji hili msingi, Jimbo Katoliki la Ifakara hapo tarehe 19 Marchi 2013, katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Yosefu mchumba wake Bikira Maria na Msimamizi wa Kanisa la Kiulimwengu, Askofu Libena akazindua Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki Ifarakara, utakaofungwa rasmi hapo tarehe 19 Marchi 2015, Jimbo Katoliki Ifakara litakapokuwa linaadhimisha Mwaka wa Tatu tangu kuundwa kwake na Baba Mtkatifu mstaafu Benedikto XVI. Ifakara ni kati ya majimbo machanga sana nchini Tanzania, lakini linaendelea kucharuka kwa maendeleo ya watu kiroho na kimwili.

Askofu Libena anasema, Mwaka wa Katekesi umekuwa ni fursa kubwa kwa Familia ya Mungu Jimboni Ifakara kuweza kupyaisha tena mafundisho tangu ya Kanisa, dhamana inayotekelezwa kuanzia kwenye ngazi ya: Familia, Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo, Vigango, Parokia na katika ngazi ya Jimbo. Lengo ni kuhakikisha kwamba, Jimbo Katoliki Ifakara litakapokuwa linaadhimisha kumbu kumbu ya miaka mitatu tangu kuundwa kwake, waamini wawe wameifahamu Katekesi kwa kina na mapana yake.

Jimbo Katoliki Ifakara linapenda kumwilisha imani katika matendo kwa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu ambayo kwa sasa inaonekana inahitaji kupewa uzito wa pekee kutokana na ukweli kwamba, kwa masuala ya afya, Jimbo limejiimarisha kwani kuna Hospitali ya Rufaa yenye vitanda 370 na idadi nzuri ya Zahanati ambazo zinaendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia utu na heshima ya binadamu.

Jimbo Katoliki la Ifakara linamiliki na kuendesha shule kadhaa za msingi, lakini kwa bahati mbaya, linamiliki Sekondari moja tu, changamoto ya kuendelea kuwekeza katika elimu, ili kuweza kuwafunda vijana wa kizazi kipya: kiroho na kimwili, tayari kulitumikia Taifa na Kanisa kwa ujumla.

Itakumbukwa kwamba, Jimbo Katoliki la Ifakara liliundwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 14 Januari 2012 na kuzinduliwa rasmi tarehe 19 Marchi 2012 na Askofu Salutarius Libena akawa ni Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki Ifakara:>>>>>bonyeza hapa soma zaidi hapa

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR