Saturday, November 29, 2014

Kikao cha Bunge chavunjika, Vurugu zatawala ukumbini

Dar/Dodoma. Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku kilivunjika baada ya vurugu kutawala ukumbini humo.
Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge hadi leo saa tatu asubuhi.
Chanzo cha vurugu ni kutokana na ugumu wa kutokukubaliana na azimio la tisa, lililolenga kumwajibisha moja kwa moja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Azimio la PAC lilitaka Waziri Muhongo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma zilizokuwa zinazomkabili ikiwamo kulidanganya Bunge.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengi wakiwa wa CCM walitaka waziri huyo asiadhibiwe na Bunge bali achukuliwe hatua na mamlaka iliyomteua.
Wakati ubishani huo ukiendelea, ikiwa imefika saa 4.42 usiku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama na Spika Makinda alimruhusu kuzungumza.
“Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo (jana) kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi,” ilikuwa ni kauli ya Mbowe.
Mara baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge wote wa upinzani walisimama na kuanza kupiga kelele kwamba wezi waondoke…tunataka fedha zirudi…tunataka fedha zirudi…vijana msilale…vijana msilale.
Wakati wabunge hao wakiendelea kuimba, wabunge wa CCM wao walikuwa wakizunguka zunguka huku wengine wakitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Hata hivyo, wabunge wa upinzani waliendelea kusimama, kuimba na kupiga makofi, huku wabunge wa CCM wakimpongeza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuruka kihunzi alichokuwa amewekewa na kamati ya PAC.
Kutokana na hali hiyo wabunge wengine walisimama vikundi vikundi, huku Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, na Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka walikuwa wakiwasihi wabunge wa upinzani wasiondoke bungeni.
Spika Makinda alisimama na kusema, “Mheshimiwa Mbowe kuondoka mapema ni mambo ya kitoto, semeni mnataka Bunge lifanye nini.”
Hata hivyo, kauli hiyo ya Makinda haikuwafanya wabunge hao kuacha walichokuwa wakikifanya, bali walibaki ndani ya ukumbi wakiwa wamesimama hadi ilipofika Saa 04:49 usiku wakati Spika Makinda aliposimama na kusema, “Waheshimiwa wabunge naahirisha kikao cha bunge hadi pale tutakaposhauriana.”
Kuvunjika kwa kikao hicho kinaweka njia panda hatima ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ambao Bunge lilikuwa halijafikia kufanya maazimio ya hatima yao.
Hoja ya baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wakitaka mapendekezo yaliyotolewa na Mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge kuhusu hatima ya Pinda na Werema yapite.
Chenge alipendekeza kuwa, “Kuhusu suala la Waziri wa Nishati na Madini lifikishwe kwa mamlaka ya uteuzi kwa hatua zaidi (wakimaanisha Rais).”
Pendekezo ambalo lilipingwa na upinzani kwa kile walichoeleza kuwa Bunge linaweza kuwawajibisha kama ambavyo limewahi fanya hivyo. Spika Makinda akijibu hoja ya Bunge kuwawajibisha alisema; “Mnajua waheshimiwa wabunge huko nyuma mawaziri walikubali wenyewe, lakini hawa wamekataa ndiyo maana tunaona haya yanatokea.”
Awali, Bunge hilo limemwachia Rais Jakaya Kikwete kufanya uamuzi wa kuwawajibisha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi baada ya kuadhimia kuwa suala lake lifikishwe kwa Rais kwa hatua zaidi.
Mjadala wa kuchukuliwa hatua kwa Maswi uliwagawa wabunge na kuwafanya kujadili kwa zaidi ya dakika 30, kufikia uamuzi huo ambao hata hivyo ulipingwa na baadhi ya wabunge.
Hata hivyo, Bunge limemwokoa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuona kuwa kauli yake aliyoitoa haikuwa na madhara yoyote hivyo hahusiki kwa vyovyote vile kwenye sakata hilo.
Hatua ya kuwashughulikia viongozi hao na wengine kuokolewa ilifikiwa baada ya mvutano mkali wa pande mbili ndani ya Bunge katika kukubaliana na mapendekezo ya kamati ya PAC.
Baada ya muda wabunge na mawaziri walioanza kuingia kwenye magari yao na kuondoka bila kujua nini kitaendelea leo.

ujasiramali ni nini

SEMINA YA MWAKA WA FAMILIA YA FANA JANA

Vijana wa Parokia za Boko na Bunju Jana waliaanza Kongamano la Ujirani Mwema, kwa semina ya mwaka wa Familia.
Semina hiyo iliongozwa na Padre Nicolaus Ngowi, Padre ambaye ni Mlezi wa Vijana Parokia ya Boko, akieleza maandalizi ya kwa vijana kuingia kwenye sakramenti ya Ndoa, ni vizuri maandalizi yafanyike vizuri, na uamuzi wa kuoa au kuolewa si vizuri uwe kwa sababu,
ikieleza zaidi alisema Familia nyingi kwa sasa zimepoteza Tuna za kikristo, Tunajua kabisa kuwa familia ni kanisa dogo la nyumbani, lakini kwa sasa Mababa wengi hawewezi hata kuongoza sala ya asubuhi, hii ni changamoto ambayo inayowafanya vijana wengi kukosa maadili mazuri.
swala la wazazi kutokuwajibika kwa watoto wao pia inachochea anguko kubwa la maadili, wababa wamesahau majukumu yao, akiwakumbusha kuwa wao ni maparoko wa familia, hawatakiwi kulegelega.......

itaendelea

Friday, November 28, 2014

YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA LEO, MBUNGE ATINGA NA BANGO KUWANIA NAFASI, AAMRIWA ASAUla

Mbunge wa Mwibara Mhe.Kange Lugola  akiomba kura za kuwania nafasi ya Mjumbe  wa Tume ya Utumishi Bungeni kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Juni 11, 2014.   Mbunge wa Mwibara Mhe.Kange Lugola akivua bango alilokuwa ameva wakati akiomba kura kwa wabunge


MATUKIO KATIKA PICHA LEO ASUBUHI BUNGENI DODOMA

1
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akiwasili leo

Wednesday, November 26, 2014

PICHA, JINSI SITTA ALIVYOWATULIZA WAPINZANI KUHUSU UFISADI WA ESROW,

Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi leo Novemba 26, 2014.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizugumza na Mbunge wa Viti Maalum Rachel Mashishanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urambo, Mh. Samuel Sitta (katikati) akiwatuliza  na baadhi ya wabunge wa Upinzani, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014

Tumeuanza Mwaka wa Watawa Duniani, 2014 - 2016


Makanisa mahalia sehemu mbali mbali za dunia, yataadhimisha Ibada ya Misa na kufanya mikesha ya sala na tafakari kama sehemu ya mchakato wa uzinduzi wa Mwaka wa Watawa Duniani, uliotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko. Waamini wanaalikwa kusali na kumwomba Roho Mtakatifu ili aweze kulikirimia Kanisa neema na baraka ili kujenga na kulipyaisha Kanisa katika maisha na utume wake
Maadhimisho ya Mwaka wa Watawa Duniani yanakwenda sanjari na Jubilee ya miaka 50 tangu Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walipochapisha Waraka kuhusu Fumbo la Kanisa, Lumen Gentium, inayojulikana kama Mwanga wa Mataifa, Kanisa kama Fumbo la Mwili wa Kristo; linaloonekana na lile lisiloonekana; umuhimu wa Taifa la Mungu katika kushiriki katika maisha na utume wa Kanissa pamoja na kukuza ari na moyo wa kimissionari.

Mama Kanisa pia anaadhimisha Jubilee ya miaka 5o tangu Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walipotoa Tamko kuhusiana na Maisha ya Kitawa: Perfect Caritatis, yaani Upendo Mkamilifu, Waraka uliowataka Watawa kupyaisha maisha yao, kwa kutoa nafasi ya kwanza katika maisha ya kiroho, mashauri ya Kiinjili, maisha ya kijumuiya pamoja na malezi makini kwa wale wote wanaotaka kujisadaka kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake.

Haya ni matukio makuu yatakayoliwezesha Kanisa kufanya tafakari ya kina katika maisha na utume wa Watawa sehemu mbali mbali za dunia. Mwaka wa Watawa Duniani unazinduliwa rasmi, Jumamosi jioni tarehe 29 Novemba 2014 kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Makuu, lililoko mjini Roma kwa Ibada na Mkesha wa Sala, kuanzia saa 1:00 Usiku. Tarehe 30 Novemba, 2014, Jumapili ya kwanza ya Kipindi cha Majilio, kutafanyika Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya.

Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume linasema kwamba, matukio haya ni muhimu sana katika uzinduzi wa Mwaka wa Watawa Duniani, kwa kujiweka chini ya ulinzi na usimamizi wa Bikira Maria, Mama wa Mungu na msimamizi wa maisha ya kitawa. Hiki ni kipindi cha matumaini, sala na tafakari ya kina kuhusu matendo makuu ya Mungu katika maisha ya Watawa wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya Mungu na jirani zao, kwa kutambua kwamba, imani ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambayo Watawa wanapenda kuwamegea na kuwashirikisha wengine.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR