Sunday, December 14, 2014

Masomo yajumapili 14 desemba 2014, juma la tatu la majilio

Jumapili, 14 Desemba 2014
Juma la 3 la Majilio

Isa 61: 1-2, 10-11;
Lk 1: 46-48, 49-50, 53-54;
1Thes 5: 16-24;
Yn 1: 6-8, 19-28

Je, uelewa wako ni upi juu ya Kristo?

Msemo “mtazamo wa kwanza ni mtazamo bora” umekuwa ni mmoja wa msema wa hatari na wenye uharibifu, katika historia ya saikolojia. “Yohane alikuja kushuhudia nuru …huyu hakuwa ile nuru” (Yn 6 – 8). Wayahudi walifurahishwa kutokana na kile Yohane alichokuwa akitenda. Kabla ya kuwa na mtu yeyote yule awe makini na mwenye kushawishi. Wanashangaa kama yeye ni masiha! … au walau nabii kama Eliya. Ingawa Yohane haitaji kujiweka mbele. Kwa umakini anawarekebisha mtazamo wao wa kwanza. Ilimpasa Yesu kujitoa sadaka mwenyewe juu ya msalaba kuwafanya wao vile alivyo.

Leo Dominika ya tatu ya Majilio inatuitwa ‘Dominika ya Furaha’, itokanayo na maneno ya antifona ya kuingilia. “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema Furahini! Bwana yu karibu” (Flp 4:4) Katika somo letu la Kwanza kuna viashiria vya furaha vilivyoongelewa na nabii kwa ajili ya liturujia hii. Vifungu vyaonyesha kuwa vyafahamika, kwasababu Yesu katika sura ya nne ya Injili ya Luka abadilisha kifungu hiki, anasoma mistari hii na kurudi kwa ndugu zake wa nazareti na anatangaza kuwa somo hili linamuhusu Yeye. Anakuja kutuponya na kutuweka huru!

Sala: Bwana Yesu, ninangojea kwa furaha ya tumaini kuupokea uponyaji na uhuru wako. Amina.

"Hata katika shlda za kazi ya malezi, shida ambazo nl kubwa zaidi aghalabu siku hizi, wazazi sharti wawafunze watoto wao kwa uaminlfu na ujaslrl katika tunu za maisha ya binadamu. Watoto sharti wakue pamoja na msimamo sahihi wa uhuru kuhusu mali ya dunia, kwa kuchagua mtindo wa maisha ulio rahisi na wa kujinyima, na kusadikishwa kabisa kwamba "binadamu ni mwenye thamani zaidi kwa hali aliyo nayo kuliko kwa kile alichonacho"" – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 37.


Tuesday, December 9, 2014

Kongamano la Ujirani Mwema Parokia ya Boko na Bunju

Kongamano la Ujirani Mwema Parokia ya Boko na Bunju

Desturi za Krismasi


Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo.
  • Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio (Italia) na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa.
  • Mapambo ya krismasi: ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemu inawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka.
  • Mti wa Krismasi - ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kama mwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi.
  • Zawadi za Krismasi - Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2. Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira.
  • Baba Krismasi / Baba Noeli

Sikuku ya Noel (Krismasi)

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.

Jina

Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii.
  • Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
  • Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".
  •  

Monday, December 1, 2014



Sunday, November 30, 2014

Maana ya Majilio katika maisha ya binadamu

Kwanza Majilio ni nini?
Majilio (pia: Adventi) ni kipindi cha liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile Kanisa Katoliki, ya Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri) kinatangulia sherehe ya Noeli na kuanza mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu kati ya siku 22 na 40.
Jina lake kwa Kilatini ni adventus maana yake ujio (wa Yesu Kristo), lakini jina la Kiswahili ni sahihi zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja zamani, anakuja kila siku na atakuja kwa utukufu mwisho wa dunia.

Maana ya Majilio katika Maisha ya Binadamu
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu ya kuishi kwa bidii ya kiroho.

Majilio katika liturujia ya Katoliki

Katika mwaka wa liturujia ya Kanisa la Katoliki, sherehe ya Noeli inaandaliwa na kipindi cha Majilio ambacho kina mambo mawili: kinakumbusha Mwana wa Mungu alivyotujilia mara ya kwanza, na papo hapo kinatuandaa kumpokea atakapotujilia tena siku ya mwisho. Kufuatana na hayo kina sehemu mbili: hadi tarehe 16 Desemba kinahusu zaidi kurudi kwa Bwana; siku nane za mwisho kinatuelekeza moja kwa moja kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Urefu wa Majilio unategemea siku inayoangukia Noeli, kwa kuwa ni lazima yawe na Jumapili nne. Hivyo basi yanaanza kwa Masifu ya Jioni ya kwanza ya Jumapili inayoangukia tarehe 30 Novemba au tarehe ya jirani zaidi; yanakwisha kabla ya Masifu ya Jioni ya kwanza ya Noeli.
Kwa jumla ni kipindi cha toba: rangi yenyewe ni zambarau; haziruhusiwi sherehe za fahari; ala za muziki na maua vinaweza kutumika kwa kiasi tu. Masharti hayo yanalegezwa katika Jumapili ya tatu kwa sababu ya furaha ya kuona tunakaribia sherehe yenyewe.
Katika kipindi hicho tunaadhimisha tumaini la Israeli lililotimizwa Yesu alipokuja katika unyenyekevu wa umbile letu; pia tunangojea arudi kwa utukufu. Kama alivyotekeleza ahadi mara ya kwanza, atazitekeleza pia mara ya pili, ingawa kwake miaka elfu ni kama siku moja tu. Kati ya majilio hayo mawili, Bwana anatujilia mfululizo kifumbo katika sakramenti (hasa ekaristi) na katika maisha ya kila siku kwa njia ya matukio na watu (hasa maskini). Basi tunapaswa kuwa tayari daima kumpokea ili siku ya mwisho tukamlaki, naye atukaribishe kwenye uzima wa milele. Pia tunapaswa kumuomba aje kutukomboa, yeye aliye tumaini letu.
Katika safari ya Majilio watu watatu wanatuongoza tukutane na Yesu: 1. Isaya nabii wa tumaini, mwenye kipaji cha kutokeza matazamio ya binadamu na kumhakikishia atatimiziwa na Mwokozi. 2. Yohane Mbatizaji, mwenye kuhimiza toba kwa kuwa tunapaswa kupindua maisha yetu ili tukutane vema na Kristo. 3. Maria, bikira aliyekuwa tayari kumpokea Masiya kwa upendo na kushirikiana naye katika kutimiza mpango wa wokovu.
Tukiwafuata hao watatu tunaweza kujipatia maadili yale yanayotuandaa kumpokea Mwokozi anapotujilia: ndiyo matunda maalumu tunayotarajiwa kuyachuma wakati wa Majilio: 1. Kukesha katika imani, sala na kutambua ishara za Bwana kutujilia katika nafasi yoyote ya maisha na mwishoni mwa nyakati. 2. Kuongoka kwa kufuata njia nyofu. 3. Kushuhudia furaha inayoletwa na Yesu kwa kuwa na upole na uvumilivu kwa wenzetu, kwa tumaini la kuwa bidii zetu zinawahisha ufalme wa Mungu wenye heri isiyo na mwisho. 4. Kutunza unyenyekevu kwa kufuata mifano ya maskini wa Injili ambao ndio waliompokea Mkombozi.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR