Saturday, August 1, 2015

Matokeo ya kura za Maoni CCM 2015

matokeo ya kura za maoni zilizopigwa nchi nzima leo kuchagua wagombea ubunge  na udiwani kwa ticketi ya nchi nzima ni kama yafuatavyo

Tuesday, July 28, 2015

UZINDUZI WA KITUO CHA HIJA BOKO

Tarehe 12/09/2015, kituo cha hija ya vijana wa jimbo kuu la Dar es salaam, kumbukumbu ya Msalaba kuombea amani ulimwenguni. kitafunguliwa Rasmi na Polycarp Pengo.

Picture ya Jengo la Kituo likiwa kwenye hatua za mwisho:





Monday, July 27, 2015

Monday, July 6, 2015

HATIMA YA TAIFA LETU: Siku saba za urais ndani ya CCM

Dodoma. Ni wiki ngumu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM). Ndivyo unavyoweza kusema kwani chama hicho kinachotawala kitafanya vikao vyake vya juu vitakavyohitimishwa kwa kumpata mgombea wake wa urais.
Mchakamchaka utaanza na kikao cha Kamati ya Maadili keshokutwa kukutana. Tayari CCM imetangaza kuwa itatumia vigezo 13 ilivyojiwekea kuwachambua wagombea 38 waliochukua na kurejesha fomu ili kupata majina ya wachache watakaopigiwa kura na mkutano wake mkuu.
Awali, kulikuwa na watangazania 42 waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM, lakini wanne kati yao hawakurejesha fomu. Kamati Kuu itakayokutana Alhamisi itakuwa na kazi ya kuwachuja hadi kubakia wasiozidi matano yatakayopigiwa kura Ijumaa ijayo katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kubaki matatu.
Katibu wa Baraza la Ushauri wa Wazee wa CCM, Pius Msekwa juzi alilieleza gazeti hili kuwa mbali na sifa hizo, suala jingine litakalotizamwa ni iwapo wagombea hao walikiuka kanuni na taratibu za uchaguzi wakati wote wa mchakato.
Majina matatu yatakayopitishwa katika kikao cha NEC ndiyo yatapigiwa kura na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM utakaokaa Julai 11 na 12 na kupata mwakilishi mmoja wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Uzoefu unaonyesha kuwa chama hicho huzingatia mambo mengi katika kufanya uteuzi, ikiwa ni pamoja na kutafuta mtu atakayeondoa makundi yaliyoundwa wakati wa uteuzi wa mgombea urais.
Baadhi ya mambo yanayotajwa kuwa yatakuwa karata muhimu katika mchujo huo ni suala la Muungano, jinsia, eneo la kijiografia, rekodi ya mtia nia na kukubalika kwa kada hasa katika kipindi hiki ambacho upinzani umeimarika. Hofu inayoonekana kukikumba chama hicho ni ya kumpata mgombea mwenye sifa na anayekubalika na atakayeweza kukabiliana vyema na yule atakayesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD.
Kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kwamba hana mgombea anayemuunga mkono kinaonyesha jinsi mchujo huo utakavyokuwa mgumu.
Kauli ya Takukuru
Kutokana na unyeti wa wiki hii, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah amesema vijana wake wako Dodoma na kuwatahadharisha wagombea wote kuzingatia sheria.
“Nawashauri wagombea wote wazingatie Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Kupambana na Rushwa, wafanye mambo kistaarabu na ambaye atakwenda kinyume, sheria itachukua mkondo wake,” alisema.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema jeshi hilo limejiandaa vizuri kwa ugeni huo mkubwa.

Tuesday, June 16, 2015

SEMINA YA VIJANA WA DEKANIA YA MT. GASPER DEL BUFFALO - MBEZI BEACH

Halmashauri ya VIWAWA Dekania Pamoja na walezi wameanda semina ya siku moja. Semina hii itafanyikia katika Parokia ya Mt. Nicolaus Kunduchi Mtongani jumamosi ya tarehe 27/06/2015.

Mada kuu kwenye Semina hii ni Kijana na Mahusiano katika familia, semina hii inatarajiwa kuanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa 9 alasiri.

Mchango ni Tshs 5000 kwa kila kijana ikiwa ni kwa matumizi ya Chakula, Vinywaji, ukumbi na malipo kwa mkufunzi(mtoa mada.

hebu kwa kifupi tuone ni yapi ambayo yataenda kufundishwa kwa kina hiyo siku,
1, Kijana ni nani
2. Mahusiano ni yapi
3. Familia ni  ipi
 ni matumaini yetu vijana wengi mtahamasika na kufika hiyo siku kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu wa kuanzisha familia mpya.

kwa mawasiliano ukiwa unataka kushiriki wasiliana na uongozi wa viwawa Dekania ya Mt. Gasper kwa number hii 0652 369 902

soma zaidi>>>>>>>

Friday, May 8, 2015

Kwanini kinaporomosha shilingi ya Tanzania?

Thamani ya Shilingi ya Tanzania imekuwa ikiporomoka kwa kasi sana ndani ya miezi mitano iliyopita
Itakumbukwa kwamba mpaka kufikia Januari mwaka jana Dola ilikuwa ikibadilishwa kwa Sh1,630 na ilikuwa ikiporomoka taratibu mpaka kufika Sh1,850 na Sh1,900 ilipofika Februari mwaka huu. Kwa sasa ni zaidi ya Sh2,000.
Kuna sababu mbalimbali zinasababisha kuporomoka kwa thamani ya shilingi.
Zipo sababu za kiuchumi ambazo pia zimegawanyika kwa kigezo cha ndani na za nje. Vilevile zipo sababu za sera na usimamizi wa sheria za nchi kuhusu masuala ya kifedha.
Sababu ya kwanza ambayo husababisha kushuka kwa thamani ya fedha ya nchini yoyote ni urari wa kibiashara (balance of trade).
Katika urari wa biashara, kinachoangaliwa ni namna nchi inavyoweza kuuza vitu nje pia inavyoagiza vitu kutoka nchi za nje. Kama nchi inatumia bidhaa nyingi za nje kuliko zile za ndani na inauza vitu nje kwa kiasi kidogo kuliko inavyoviagiza basi thamani ya fedha ya nchi hiyo lazima ishuke kwa kasi.
Kwa Tanzania bidhaa nyingi tunazozitumia ni za nje hivyo tunahitaji zaidi Dola ili tuweze kununua bidhaa hizo katika soko la dunia. Hii inapekea hitaji la shilingi liwe dogo ikilinganishwa na hitaji la Dola hivyo thamani ya Dola inakuwa juu kuliko ya Shilingi ya Tanzania.
Suala jingine linaloweza kuathiri thamani ya fedha ya nchi yoyote ni masuala ya uwekezaji kutoka nje yaani Foreign Direct Investment (FDI).
Uwekezaji wa nje ukiongezeka kwa kiasi kubwa husababisha thamani ya fedha ya nchi husika kupanda kwa sababu hitaji lake linakuwa kubwa kwa wawekezaji ambao wanaendesha miradi yao kwa gharama kubwa kwa fedha ya nchi husika.
Hatujapata bado tamko la serikali ama takwimu zozote zinazoonyesha kama uwekezaji kutoka nje umepungua ama wawekezaji wamepunguza mitaji lakini ni moja kati ya sababu ambazo za kushuka ama kupanda kwa thamani ya fedha katika nchi husika.
Thamani ya fedha inaweza pia kuathiriwa na uwekezaji ambao unavuka mipaka ya nchi na sekta mbalimbali kwa lugha ya kimombo; portfolio Investment.
Hii ni aina ya uwekezaji ambao huendeshwa kwa mitaji ya hisa kwa watu kutoka katika mataifa mbalimbali kwa mfano mtu anaweza kuwa ni Mtanzania lakini akawa anahisa katika kampuni ya Uingereza.
Kukiwapo na portifolio investment nyingi hapa kwetu hisa zake zitakuwa zinauzwa kwa shilingi hivyo watu wa mataifa mbalimbali watahitaji kuinunua ili waweze kuwekeza.
Uwekezaji wa namna hii hapa kwetu upo kwa kiasi kidogo sana hivyo inasababisha hitaji la shilingi kwa watu wa mataifa mengine lisiwe kubwa kitu ambacho kinashusha thamani ya fedha yetu.
Nchi ambazo taasisi zake za kifedha zinatoa riba kubwa kwenye mitaji ya fedha ya wateja wake huvutia watu wengi kununua fedha ya nchi hiyo kwa ajili ya kunufaika.
Kwa bahati mbaya hapa nchini suala la riba limekuwa linanufaisha upande mmoja yaani taasisi za kifedha. Taasisi za fedha zinatoza wateja wake riba kubwa wakati mwingine zaidi ya asilimia 13 kwenye mikopo ambayo wateja wanakopa kutoka katika taasisi hizo.
Wakati huohuo, watu ambao wanawekeza fedha zao kwenye taasisi hizo kupitia mfumo wa akaunti ya muda maalumu ama fixed deposits, hupewa ongezeko la riba kwa kiasi kidogo, mara nyingi ikiwa ni chini ya asilimia sita.
Suala hili linaathiri thamani ya fedha ya Tanzania kwa sababu watu ambao wanawekeza katika mitaji ya fedha wanapata ongezeko dogo la riba.
Sababu ya nje ni kuimarika kwa Dola ya Marekani. Taarifa ya mwenendo wa Dola ya Marekani ya Oktoba 2014, inaonyesha kuwa imekuwa ikiimarika na inaweza ikaendelea kufanya hivyo mpaka mwishoni mwa mwaka 2015.
Wachambuzi wa uchumi wa kimataifa wanahusisha kuimarika kwa Dola ya Marekani na mambo ambayo tayari nimeyaainisha.
Moja ni kwamba baada ya mtikisiko wa kiuchumi (2008 – 2009) uwekezaji katika mitaji ya hisa kwa watu wa mataifa mbalimbali umerejea katika hali yake.
Benki Kuu ya Marekani imerejesha ongezeko la riba katika mitaji ya fedha hivyo watu wananua dola zaidi ili waweze kunufaika kwa kuziwekeza kupitia benki.
Marekani kwa sasa ni nchi ya kwanza duniani kwakuwa na uwekezaji kutoka nje ya nchi. Pia, ongezeko la uzalishaji wa mafuta katika nchi hiyo ambao umepunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje umesababisha pia ongezeko la thamani ya dola kwani watu wa nchi hiyo wanahitaji fedha za nchi nyingine kama ilivyokuwa awali.
Sababu ya mwisho na muhimu ni suala la uwezo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuweza kusimamia kikamilifu sera, sheria na kanuni za fedha.
BOT inapaswa kusimamia matumizi ya fedha za Tanzania kwani kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2006, shilingi ya Tanzania ndio fedha halili kwa malipo ya bidhaa na huduma hapa nchini.

Thursday, May 7, 2015

MVUA ZAENDELEA KUWATESA WATU DAR



Baada ya mvua ya kubwa ya kama masaa mawili mfululizo,maeneo mengi jijini Dar yamejaa maji na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili.Pichani ni eneo la Morogoro Road
Barabara ya Bibi Titi Mohamed mambo yalikuwa namna hii,wenye magari madogo walipita kwa staili ya maji ya shingo

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR