Monday, October 26, 2015

MATOKEO YA URAISI MAGUFULI ANAONGOZA KWA ASILIMIA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka majimbo matatu ya Makunduchi na Paje huko Zanzibar na Lulindi Mkoani Mtwara kwa Tanzania Bara.
Akitoa matokeo hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstahafu DAMIAN LUBUVA amesema katika majimbo hayo katika wagombea wanane mgombea wa Chama cha Mapinduzi DR. JOHN MAGUFULI alikuwa anaongoza akifuatiwa na Bwana EDWARD LOOWASA,mgombea wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia CHADEMA chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.
Kwa mujibu wa matokeo hayo katika Jimbo la Makunduchi DR. MAGUFULI alipata zaidi ya kura 8,400 sawa na asilimia 81 na Bwana EDWARD LOWASA alipata zaidi ya kura 1,700 sawa na asilimia 17.
Katika jimbo la Paje DR. MAGUFULI alipata zaidi ya kura 6,000 sawa na asilimia 75 ya kura halali na Bwana LOWASA alipata zaidi ya 1,800 sawa na asilimia 23.6 ya kura zote halali.
Kwa upande wa Jimbo la Lulindi Mkoani Mtwara DR. MAGUFULI alipata zaidi ya kura 31,000 sawa na asilimia 71.2 ya kura halali wakati Bwana LOWASA alipata zaidi ya kura 11,500 sawa na asilimia 26 ya kura.

JIMBO LA BUYUNGU KIGOMA, MATOKEO HAYA HAPA

Ndugu Bilago Kasuku Samson ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia chama cha  CHADEMA/UKAWA

CCM WAMETETEA JIMBO LA CHALIZE MSHINDI NI RIDHWANI KIKWETENA HAWA GHASIA MTWARA VIJIJI ASHINDA

Ridhwani Kikwete (CCM) amefanikiwa kutetea kiti chake cha Ubunge wa Jimbo la Chalinze. Vilevile Hawa Ghasia (CCM,Mtwara Vijijini) na Shukuru Kawambwa (CCM,Bagamoyo) wamefanikiwa kutetea viti vyao vya Ubunge.

BUNDA TAYARI MATOKEO YAMETANGAZWA NI EASTER BULAYA

Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini Ester Bulaya CHADEMA ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo na kumuangusha Steven Wasira aliyekuwa waziri wa serikiali ya awamu ya nne

MATOKEO YA URAIS KUTOKA TUME YA UCHAGUZI JIMBO LA BUMBULI, MKOANI, CHAMBANI

4. Jaji Lubuva Matokeo ya Urais Jimbo la Bumbuli Kura: 44,011
John Pombe Magufuli (CCM): 35,310
Edward Lowassa (Chadema): 7,928


5. Jaji Lubuva Matokeo ya Urais Jimbo la Mkoani Kura: 11,245
John Pombe Magufuli (CCM): 3,341
Edward Lowassa (Chadema): 7,368


6. Jaji Lubuva Matokeo ya Urais Jimbo la Chambani Kura: 6,454
John Pombe Magufuli (CCM): 818
Edward Lowassa (Chadema): 5,319'


7. Jaji Lubuva Matokeo ya Urais Jimbo la Kibaha Mjini Kura: 62,102
John Pombe Magufuli (CCM): 34,604
Edward Lowassa (Chadema):25,448
 

8. Jaji Lubuva Matokeo ya Urais Jimbo la Kiwani Kura: 6,459
John John Pombe Magufuli (CCM): 1,661
Edward lowassa (Chadema): 4,229


9.  Jaji Lubuva Matokeo ya Urais Jimbo la Kiwengwa Kura: 4,970
John Pombe Magufuli (CCM): 3,317
Edward Lowassa (Chadema): 1,104


TUNDUMA NAO WAMESHAPATA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MBUNGE WAO

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Mwakajoka Frank wa Jimbo la Tunduma (Mbeya) ametangazwa rasmi mshindi katika jimbo hilo, hongereni sana

LINDI MJINI MATOKEO TAYARI MBUNGE ALIYECHAGULIWA NI

 Jimbo la Lindi Mjini, CCM wameshinda Mbunge ni  Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR