Tuesday, June 18, 2013
Papa atoa wito: Semeni ndiyo kwa maisha na hapana kwa Kifo
Papa Fransisko ametoa wito kwa watu wote kuyatetea maisha na hapana kwa kifo. Kusema ndiyo kwa maisha na kukataa kila kitendo kinachotaka kukatisha uhai , kusema hapa kubwa kwa kifo. Papa alitoa wito huu wakati wa hotuba yake siku ya Jumapili asubuhi, ambamo Mama Kanisa aliadhimisha SIKu ya Injili ya Maisha “ Evangelium Vitae” .
Katika homili yake aliyoitoa mbele ya umati wa watu wapatao 200,000 waliofurika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , kuhudhuria Ibada ya Misa iliyoongozwa na Papa, na pia kwa ajili ya sala Ya Malaika wa Bwana, ibada na sala zilizofanyika katika mtazamo wa maadhimisho Mwaka wa Imani, siku ililega zaidi majitoleo ya Injili ya Maisha.
Katika homilia yake , Papa Francis, alitafakari Maandiko Matakatifu yanavyotuambia mara kwa mara, jinsi Mungu Mmoja Hai, ndiye mwenye kutoa maisha.
Hata hivyo, alisema kwamba "mara nyingi, watu hawachagui maisha, hawaikubali Injili ya Maisha bali hujiachia wenyewe kuongozwa na itikadi na njia yapotofu katika kufikiri, zenye kuwekea maisha kibambaza, njia zisizo heshimu maisha, kwa sababu wamekubali kuongozwa na nguvu za ubinafsi katika utafutaji wa maslahi faida, mamlaka na kujijifurahisha , na si kwa ajili ya upendo kwa wengine , au kujali manufaa ya wengine.
Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa, watu wana ndoto za kujenga upya "Mnara wa Babeli", mji wa mtu asiyekuwa na Mungu. Wanaamini kwamba kumkataa Mungu, kuukataa ujumbe wa Kristo na Injili ya Maisha, huwaongoza kwa namna fulani katika furaha, kuwa na uhuru kamili wa kutimiza malengo yao ya kibinadamu. Na kama Kama matokeo yake , Papa aliendelea, Mungu aliye hai huondolewa na badala yake huwekwa miungu mbadala mfululizo ya kibinadamu ambayo hulewesha mtu katika uhuru bandia , ambao mwisho wake hujenga aina mpya za mfumo wa utumwa na kifo.
Papa alimalizia homilia yake na wito kwa waamini, kuyaonamadhara hayo ni hivyo waseme Ndiyo kwa Mungu ambaye ni Upendo. Ndiyo kwa Maisha ya kushikamana na Mungu ndiye uhuru wa kweli na hamfadhaishi mtu.
Mara baada ya Ibada ya misa Takatifu, Papa aliongoza sala ya Malaika wa Bwana. Katika hotuba yake fupi, Papa alielekeza mawazo yake katika mifano ya watu walioyatetea maisha kikamilifu, akiangalisha katika tukio la Siku ya Jumamosi ambamo Mama Kanisa alimtagaza kuwa Mwenye Heri , baba wa watoto saba wa Capri Italy, aliyeuawa katika kambi za msongamano za Nazi mwaka 1944, ambaye aliyaokoa maisha mengi katika kambi hiyo , kabla ya kupoteza yake mwenyewe.
Papa pia aliitumia nafasi hiyo kusalimia washiriki wa Mkutano wa hadhara wa wanachama wa Harley-Davidson, kwa ajili ya kutumia kwa miaka 110, tangu kutengenezwa kwa pikipiki, yenye nembo hiyo ya Harley Davidson, ambayo inajulikana kuwa aina ya kipekee na mashuhuri Marekani. Kwa ajili ya sherehe hii zaidi ya wapanda pikipiki 100,000, walikusanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki hii. Kati yao 1400 wakiwa na pikipiki zao , walibarikiwa na Papa wakati huo wa sala ya Malaika wa Bwana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
No comments:
Post a Comment