Tuesday, January 13, 2015

Mkutano Mkuu wa VIWAWA 31/01/2015

Mapendo sana!!!!!!
Ule Mkutano Mkuu wa VIWAWA, Parokia unafanyika tena mwaka huu, tukiwa na kumbukumbu nzuri ya Mafanikio yaliyotokana na Mkutano wa Tarehe 01/06/2013.


Read More

Viongozi wa Kigango cha Boko wakati wa Mkutano mkuu 2013

Viongozi wa Kigango cha Mt. Rafael Mbweni Malindi wakati wa Mkutano Mkuu 2013

viongozi wa VIWAWA  kigango cha Mt. Fransis wa Asizi Mbweni wakati wa Mkutano Mkuu 2013
 Maadhimio ya Mkutano huo yalileta mafanikio makubwa sana kwenye Chama chetu, tukikumbuka ziara ya Uinjilishaji ambayo ilikuwa yakihistoria, Paroko Cup na Dekania Cup yote yalikuwa ni matunda ya umoja na mipango ambayo tulifanya kwa Pamoja. Mungu awabariki sana wote walishiriki na kuyafanikisha yale yote tuliyofanya.

Mwaka huu tena tunafanya Mkutano mkuu wa Mwazo wa Mwaka, Baada ya Mwaka jana kushindwa kufanya na kupelekea chama chetu kuyumba
"tunatumwa tena kwenda shambani tukayasafishe Magugu ili shamba libaki safi kabisa tukiwa tunaamini tunatumwa na Baba na ni sisi vijana wenye nguvu".
Mkutano huu utafanyikia Parokiani Boko kuanzia saa 4:00 asubuhi Mpaka saa 8:00 mchana, hivyo ukiwa kama kiongozi wa Jumuiya au Kijana Mshiriki mzuri wa Jumuiya, Kiongozi wa VIWAWA Kigango au Mwanachama Hai wa VIWAWA unakaribishwa kushiriki nasi katika mkutano huu.
Vitu Muhimu, Mada Jadiliwa
Mkutano huu utakuwa na sehemu kuu Tatu
a) Utangulizi
b)Tasmini ya kipindi kilichopita
c)Mipango ya Mwaka 2015-2016 na utekelezaji wake.
Hivyo ukiwa kama mjumbe ni kipindi cha wewe kuanza kufanya tasmini yako ili uweze kuiwakilisha hiyo siku pamoja na mapendekezo ya  mambo ambayo unapenda yafanyike kwa kipindi kijancho

Tunarejea ujumbe wetu wa mwaka huu unaosema "Kijana inakupasa uwe Mfano bora ushiriki kikamilifu Sakramenti"
niwatakieni maandalizi mema!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR