15
FEBRUARY
SOMO 1. Law. 13:1-2, 44-46
Somo katika kitabu cha Walawi
Bwana alinena na Musa na Haruna, na kuwaambia, mtu atakapokuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king'aacho, nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmoja wapo; yeye ni mtu mwenye ukoma, yu najisi; na kuhani hana budi atasema kuwa yu najisi; pigo lake li katika kichwa chake. Kisha mwenye ukoma aliye na pigo ndani yake, nguo zake zitararuliwa, na nywele zake za kichwa chake zitaachwa wazi, naye atafunika mdomo wake wa juu, naye atapiga kelele, ni najisi. Siku zote ambazo pigo li ndani yake, yeye atakuwa mwenye unajisi; yeye yu najisi; atakaa peke yake; ,makazi yake yatakuwa nje ya marango
somo 2. 1Kor. 10:31-33, 11-1.
Somo katika Waraka wa kwanza wa mtume Paulo kwa Wakorintho
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu; vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisatake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa. mnitafute mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.
.
INJILI.Mk. 1:40-45.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Marko.
YMtu mwenye ukoma akaja kwa Yesu, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, ukitaka, waweza kunitakasa. Naye akamhurumia, akanyoosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, nataka, takasika, Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, akamwambia, Angalia, Usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao. Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila mahaliSomo katika Injili ilivyoandikwa na Marko.
No comments:
Post a Comment