Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Prosper Balthazar Lyimo, kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Arusha, Tanzania.
Wasifu wake
Askofu mteule Prosper Balthazar Lyimo alizaliwa Kyou – Kilema, Jimbo Katoliki la Moshi, tarehe 20 Agosti 1964 . Baada ya masomo yake ya shule ya msingi huko Maua na Arusha, alijiunga na Seminari ndogo ya Jimbo Katoliki Arusha. Alipata masomo yake ya Falsafa kwenye Seminari kuu ya Kibosho, iliyoko Jimbo Katoliki la Moshi na masomo ya Taalimungu alipata Seminari kuu ya Kipalapala, iliyoko Jimbo kuu la Tabora.
Baada ya majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa Jimbo kuu la Arusha kunako tarehe 4 Julai 1997. Tangu wakati huo amekuwa ni mlezi katika Seminari ndogo ya Jimbo kuu la Arusha kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 1999. Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2004 alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo kuu la Arusha. Kunako mwaka 2004 hadi mwaka 2007 alipelekwa na Jimbo kwa ajili ya masomo ya juu mjini Roma, kwenye Chuo kikuu cha Kipapa cha Urbaniana. Kunako mwaka 2007 hadi mwaka 2008 alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo kuu la Arusha
Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2011 Askofu mteule Prosper Balthazar Lyimo, alitumwa na Jimbo kuu la Arusha kwa ajili ya masomo ya juu nchini Canada na huko akajipatia shahada ya uzamivu kutoka katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Paul, kilichoko mjini Ottawa. Na kunako mwaka 2011 alirejea nchini Tanzania na kupangiwa kazi ya kuwa Katibu mkuu na Mkuu wa Mahakama ya Jimbo kuu la Arusha.
Askofu mteule Lyimo kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Mahakama ya Kanisa Jimbo kuu la Arusha.
Read More.........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
No comments:
Post a Comment