MAANA YA MAISHA
Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.
Limekuwa suala kuu la udadisi kwa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na kiutamaduni.Maana ya maisha imechanganyikana kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili, hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya maisha haya.
Michango ya sayansi kawaida ni ya moja kwa moja na inaeleza uhalisia kutokana na mambo yanayopimika kuhusu ulimwengu; sayansi inatoa muktadha na mipaka kwa mazungumzo kuhusu mada zinazohusika.
Mbadala ni mtazamo wa kifalsafa unaokabili swali: "Ni nini maana ya maisha 'yangu'?" Thamani ya swali linalohusu kusudi la maisha huweza kuwiana na kuupata ukweli wa mwisho, au hisia za umoja, au hisia ya utakatifu.
Uchunguzi wa kisayansi
Kwamba sayansi inaweza kutusaidia kuelewa zaidi kuhusu masuala ya msingi (kama vile maana ya maisha) ni suala linalozua mabishano mengi katika jamii za sayansi na falsafa ya sayansi.Hata hivyo, sayansi inaweza kutupa muktadha fulani na huiweka baadhi ya mipaka ya mazungumzo kuhusu mada kama hizo.
Umuhimu wa kisaikolojia na thamani katika maisha
Sayansi huenda ikashindwa kutuambia nini ni cha thamani maishani, lakini baadhi ya fani zake hugusia maswali yanayohusiana: watafiti katika saikolojia chanya hutafuta sababu zinazoleta hali ya ndani ya kuridhika na maisha. kujihusisha vikamilifu katika shughuli, kufanya mchango zaidi kwa kutumia vipawa vya kibinafsi,
Aina moja ya mfumo wa thamani iliyopendekezwa na wataalamu wa elimunafsia ya jamii, iitwayo kwa upana "Nadharia ya Kupambana na Mambo ya Kutisha", inasema kwamba maana yote ya binadamu inatokana na hofu ya msingi ya kifo, ambapo maadili yanachaguliwa yanapotusaidia kuepukana na kumbukumbu ya kifo.
Sayansi ya niurolojia imetunga nadharia ya malipo, raha na msukumo katika masuala ya kimwili kama shughuli za kupitisha ujumbe za kiniuro. Ikiwa mtu anaamini kwamba maana ya maisha ni kufanya raha ziwe nyingi iwezekanavyo, basi nadharia zinatoa utabiri unaozidi kuongezeka, kuhusu jinsi ya kufanya ili kufanikisha hilo.
Somo la kijamii linapima thamani katika ngazi ya kijamii kwa kubuni nadharia kama vile nadharia ya thamani kanuni, anomi, n.k.
Asili na hali ya maisha ya kibiolojia
Kufanya kazi kwa abayojenesisi hakueleweki kwa ufasaha: nadharia mashuhuri ni pamoja na nadharia ya dunia ya RNA (vitoaji aina sawa katika makao ya RNA) na nadharia ya dunia ya chuma-sulfuri (umetaboli bila Jenetikia). Nadharia ya mabadiliko ya viumbe haijaribu kuelezea asili ya uhai, bali mchakato ambao viumbe tofauti vimepitia katika kipindi chote cha historia kupitia mabadiliko ya ghafla ya kijenitikia na uteuzi wa kiasili Wakati wa mwisho wa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu wa mabadiliko ya viumbe unaotegemea jeni hasa, wanabiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig, miongoni mwa wengine, wanahitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu.Ingawa wanasayansi wameyachunguza maisha yalivyo duniani, kuyafafanua bayana bado ni changamoto. Kimwili, mtu anaweza kusema maisha "hula entirofi hasi" ambayo walio hai wanapunguza entirofi yao ya ndani kwa gharama ya aina fulani ya nishati inayochukuliwa ndani kutoka mazingira.
Wanabiolojia kwa jumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za kimetaboliki hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu uhai kuendelea kwa vizazi vingi. Kwa kawaida, maumbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za kijenitikia, hivyo huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu marekebisho kupitia mabadiliko ya kimwili. Sifa hizo huongeza nafasi ya kuishi ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo.
Viwakala visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa jumla havitazamwi kama viumbe kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendesha shughuli za kimetaboliki. Pambano hilo ni tatizo, ingawa baadhi ya vimelea na visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi maisha ya kujitegemea.
Astrobiolojia inajihusisha na masomo ya uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe hai katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa vingine visivyo DNA.
Asili na hatima ya ulimwengu
Ingawa dhana ya Mlipuko mkuu ilipozinduliwa mara ya kwanza ilipambana na shaka kwa wingi, shaka iliyochangiwa na uhusiano na imani ya dini ya uumbaji, imekuja kuungwa mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea. Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza kuelezea tu ulimwengu ulivyokuwa mapema sekunde 10 baada ya kutokea. Wanafizikia wengi wamedadisi nini inaweza kuwa imetangulia, na jinsi ulimwengu ulivyoanza. Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko mkuu ulitokea kiajali, na kanuni ya kianthropiki inapozingatiwa, mara nyingi hutafsiriwa kuashiria uwepo wa ulimwengu maridhawa.
Hata hivyo, haijalishi jinsi ulimwengu ulivyokuja kuwepo, hatima ya binadamu katika ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu utaishi muda huo wote - maisha ya kibiolojia hatimaye yatashindwa kujiendeleza.
Maswali ya sayansi kuhusu akili
Hali ya kweli na asili ya fahamu na akili yenyewe pia vinajadiliwa sana katika sayansi. Suala la hiari pia linaonekana kuwa na umuhimu wa msingi. Masuala hayo hupatikana zaidi katika nyanja za sayansi koginitivu, niurolojia na falsafa ya akili, ingawa baadhi ya wanabiolojia wa mabadiliko ya viumbe na wanafizikia wa kinadharia pia wameliashiria sana suala hilo.Kwa upande mwingine, wanasayansi kama Andrei Linde wanadhani kwamba fahamu, kama nafasi-wakati, huenda ikiwa na ngazi zake za ndani za uhuru, na kwamba maoni ya mtu binafsi yanaweza kuwa halisi kama (au hata kuliko) vifaa tunavyoweza kuvigusa na kuviona.
Nadharia ambazo hazijabainishwa za fahamu na nafasi-wakati zinaelezea kuhusu fahamu katika kuelezea "nafasi ya vipengele vyenye fahamu", mara nyingi zikijumuisha idadi kubwa ya mitazamo ya ziada.
Nadharia za sumakuumeme za fahamu zinatatua tatizo lenye vipengele vingi la fahamu kwa kusema eneo la sumakuumeme linalotokana na ubongo ndilo hasa linalobeba fahamu zoefu. Hata hivyo kuna kutokubaliana kuhusu kutekelezwa kwa nadharia kama hiyo inayohusu utendaji kazi kwingine kwa akili.
Nadharia za akili za kikwontamu hutumia nadharia ya kwontamu kuelezea baadhi ya sifa za akili.
Ikitegemea hoja ya maelezo ya akili yasiyoweza kugusika, baadhi ya watu wamependekeza uwepo wa fahamu ya kikozmiki, wakidai kwamba fahamu kwa kweli ndiyo "msingi wa yote kuwepo". Wanaounga mkono mtazamo huo wanaelezea matukio yasiyo vya kawaida, hasa uwezo wa kuhisi usio wa kawaida na uwezo wa kuyasoma mawazo, kama ushahidi wa uwepo wa fahamu ya juu isiyoeleweka. Katika matumaini ya kuthibitisha uwepo wa mambo hayo yasiyokuwa ya kawaida, wanaelimunafsia wa mambo yasiyo ya kawaida wamefanya majaribio mbalimbali. Uchambuzi unaoangalia mambo yote yaliyopo unaonyesha kuwa idadi ya wenye nguvu zisizo za kawaida (ingawa ndogo sana) kwa ulinganishaji imebaki thabiti. Ingawa baadhi ya wachambuzi wakosoaji wanahisi kuwa somo la elimunafsia isiyo ya kawaida ni sayansi, hawaridhishwi na matokeo ya majaribio yake.
Wanaochunguza mambo haya upya, wanabaki na wasiwasi kwamba matokeo yanayoonekana kuwa na mafanikio huenda yakawa yanatokana na utaratibu mbaya, na watafiti wasiokuwa na mafunzo ya kutosha, au mbinu hafifu.
No comments:
Post a Comment