Thursday, January 7, 2016

SUMATRA WAKARIBISHA MAONI YA WANANCHI JUU YA NAULI ZA MABASI YAENDAYO KASI



MAMLAKA ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajia kukusanya maoni ya wananchi juu ya viwango vya nauli za mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri wa haraka Jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa SUMATRA kwa vyombo vya habari kwenda kwa wananchi  ambapo ofisi hiyo itawaalika wadau wote wa usafiri hususani wananchi kuchangia maoni kwenye mkutano utakao fanyika januari 5 kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 na nusu asubuhi.

Mamlaka  pia inapokea maoni ya wananchi kupitia anuani ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo ambayo ni S.L.P 3093 au kwa barua pepe ambayo info@sumatra.go.tz ambapo kabla ya kufikia uamuzi wadau wanatakiwa kutoa maoni ya kuridhia viwango vya nauli  kwa mujibu wa sheria ya Sumatra.

Maoni ya maandisi yatapokelewa kwenye ofisi ya Mkuregenzi Mkuu iliyopo Jengo la Mawasiliano House Makutano ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Nkumo kuanzia Saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri mwisho wa kupokelewa maoni hayo ni Januari 13 mwaka huu.

Mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kampuni ya UDA-RT inayolenga kutoa huduma ya mpito ya usafirishaji jijini Dar es Salaam katika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa Dart.

Maombi yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ni Safari kwenye njia za pembeni (feeder route) shilingi 700 ,safari kwenye njia kuu (trunk route) shilingi 1200 na njia zote mbili ni 1400 ambapo wanafunzi watalipa nusu nauli anayotoa mtu mzima.

HARMONIZE AMEAMUA KUCHORA TATOO YA BOSS WAKE

Msanii wa label ya WCB anayekuja juu kwa sasa, Harmonize ameamua
kuuthibitishia ulimwengu kuwa anajivunia kuwa mtoto wa kimuziki wa staa
wa Tanzania, Diamond Platnumz kwa kuchora tattoo yenye picha yake na
kuandika a.k.a ya Boss wake iliyozua utata hivi karibuni ‘Simba’.
h n d
Hiki ndicho alichokiandika Harmonize kwenye picha aliyoipost Instagram
kuelezea sababu za kuchora tattoo hiyo:
Harmonize tattoo
Harmonize tattoo

/“Katika Maisha Yangu Sikuwahi Kuwaza Kuwa Itatokea Siku Nikajichora
Tatoo But Diamond Nimtu Mwenye Mchango Mkubwa Sanaaaa Katika Maisha
Yangu Leo Hii Mimi Ninathaminika Kutoka Kwenye Kunyanyasika
Ninaheshimika Kutoka Kwenye Kudhalaulika Nimekuwa Maarufu Na Kupata
Uthamani Mkubwa Kupitia Yeye Siotu Kwa Kipaji Nilicho Nacho Kwani
Wangapi Wanavipaji…??? Naisaidia Familia Yangu Kwa Kile Nikipatacho
Sihaba Akiwa Na Mchango Wake Mkubwa Sana…… Lakini Mwisho Wasiku Haya Ni
Maisha Nahii Ni Dunia Inamambo Mengi Sanaa Hasa Sisi Vijana Ambao
Niwepesi Wa Kujisahau Kinaweza Tokea Kitu Kidogo Sanaa Ukasahau Wema Na
Fadhira Ulizotendewa, Lakini Pia Mungu Ndio Katukutanisha Na Karibia
Watu Wengi Wanajua Tumekutanaje Kwamana Nimekuwa Nikiulizwa Katika
Vyombo Vya Habari Tofauti Tofauti So Watu Wengi Wanajua Tulivyo Kutana
But Hakuna Anaejua Tutaachana Vipi kwamana Sisi Ni Binadamu Kuna Kifo
Leo Na kesho Huwezi Jua Yawanadamu Ni Mengi Siamini Kuwa Binadamu Wote
Duniani Wanafurahia Mahusiano Na Ukaribu Wetu Na Huwezi Shindana Na
Binadamu Ukijua Yambele Wenzio Wanajua Yanyuma Ndio Mana Yakujichora
Hiii Picha Yake Amabayo Haitofutika Hadi Naingia Kaburini Hata ikitokea
Hatupo Pamoja Nikiitazama Hii Picha Itabaki Kama Kumbu Kumbu Na Heshima
Yangu Kwake Hadi Siku Yangu Ya Mwisho Haya Ni Maamuzi Yangu Binafsi…..”/

Uganda yaongoza orodha ya nchi zinazoridhika zaidi kimapenzi

081512-health-std-Gonorrhea-kissing-couple-diseasesUganda imeongoza orodha ya nchi duniani ambazo wananchi wake wanaridhika zaidi kimapenzi.

Utafiti huo ulifanywa na kampuni inayotengeneza condom, Durex na kuhusisha watu 26,000 kuanzia miaka 16 katika nchi 26.
Katika utafiti huo walibaini kuwa ni watu 44 pekee ndio wanaoridhika na maisha yao ya mapenzi. Uganda, Switzerland na Hispania ndio zimeongoza orodha ya watu wanaoridhika zaidi kimapenzi. Utafiti huo ulibaini kuwa waganda 5 kati ya 10 hushiriki tendo hilo walau kwa saa moja kila wiki. Hii ilionekana kuwa ni juu zaidi kwa watu kushiriki tendo hilo duniani.
Tanzania haipo kwenye orodha hiyo.
Hii ni orodha nzima:

1. Uganda
2. Switzerland
3. Hispania
4. Italia
5. Brazil
6. Ugiriki
7. Uholanzi
8. Mexico
9. India
10. Australia
11. Ujerumani
12. China

Isome Orodha ya Albamu 10 zilizouza zaidi Marekani (USA) mwaka 2015

Adele-2015-press-Alasdair-McLellan-XL-billboard-650-2Kampuni ya Nielsen Music imetoa orodha ya album 10 zilizouza zaidi mwaka 2015 nchini Marekani.

Imeanza kuangalia mauzo ya album hizo kuanzia Dec. 29, 2014 hadi Dec. 31, 2015. Hii ni orodha nzima:
1 Adele, 25 – 8,008,000
2 Taylor Swift, 1989 – 3,105,000
3 Justin Bieber, Purpose – 2,225,000
4 Ed Sheeran, X- 2,206,000
5 The Weeknd, Beauty Behind the Madness – 2,045,000
6 Drake, If You’re Reading This It’s Too Late – 1,919,000
7 Meghan Trainor, Title – 1,795,000
8 Sam Smith, In the Lonely Hour- 1,741,000
9 Sam Hunt, Montevallo – 1,378,000
10 Fetty Wap, Fetty Wap- 1,295,000

BONDE LA MTO MSIMBAZI(bomoa bomoa kuendelea)

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema kazi ya ubomoaji nyumba zilizoko katika Bonde la Mto Msimbazi itaendelea leo katika maeneo ambayo hayako kwenye zuio lililotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi Mkuu wa NEMC,  Bonaventure Baya,   alisema zuio lililopo mahakamani linahusu nyumba 681 tu, hivyo wataendelea na kazi  katika maeneo yote  yaliyobaki.
Alisema mpango wa ubomoaji wa majengo  katika bonde hilo ulianzishwa na serikali kwa lengo la kusafisha bonde na mto huo na mazingira yanayozunguka ili kunusuru maisha ya wananchi kupanua uwezo wa mto huo.
“Bonde la Msimbazi halifai kwa ujenzi wa makazi kwa kuwa kuna madhara ambayo ni pamoja na mafuriko ya mara kwa mara, uchafuzi wa mto huo unahatarisha afya za wananchi kutokana na taka nyingi na zikiwemo majitaka toka viwandani na makazi ambayo hutupwa katika bonde hilo,” alisema Baya.
Akizungumzia sababu ya Serikali kufanya ubomoaji huo alisema, Serikali ilishachukua hatua mbalimbali katika miaka ya nyuma ikiwemo ya kuwapa waathirika wa mafuriko viwanja  mbadala  katika eneo la Mabwepande pamoja na vifaa vya ujenzi, lakini baadhi ya wananchi waliviuza na kurejea mabondeni.
“Zoezi hili ni la kitaifa litafanyika kwa nchi nzima kwa awamu mbalimbali kwa kuwa kuna uharibifu mkubwa unaondelea hususani katika mito kutokana na uchimbaji holela wa mchanga na madini, utupaji majitaka toka katika makazi na viwandani hali inayosababisha maji ya mito kuwa na sumu,” alisema Baya.
Mkurugenzi huyo wa NEMC, alizitaja sekta za Serikali zinazohusika katika kazi hiyo ni pamoja na taasisi yao ambayo ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mipango Miji, halmashauri za manispaa za Dar es Salaam,  Idara ya Misitu, Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Usalama wa Taifa.
Wakati hayo yakiendelea jana maofisa wa NEMC waliuweka alama ya X katika nyumba 300 kuanzia eneo la Kipawa hadi Gongolamboto.

HIVI NI NANI ANAYAEIJUA SIRI YA DUNIA HII NA KUNA MAISHA BAADA YA HAPA DUNIANI

MAANA YA MAISHA


Maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?
Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.
Limekuwa suala kuu la udadisi kwa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na kiutamaduni.
Maana ya maisha imechanganyikana kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili, hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya maisha haya.
Michango ya sayansi kawaida ni ya moja kwa moja na inaeleza uhalisia kutokana na mambo yanayopimika kuhusu ulimwengu; sayansi inatoa muktadha na mipaka kwa mazungumzo kuhusu mada zinazohusika.
Mbadala ni mtazamo wa kifalsafa unaokabili swali: "Ni nini maana ya maisha 'yangu'?" Thamani ya swali linalohusu kusudi la maisha huweza kuwiana na kuupata ukweli wa mwisho, au hisia za umoja, au hisia ya utakatifu.

Uchunguzi wa kisayansi

Kwamba sayansi inaweza kutusaidia kuelewa zaidi kuhusu masuala ya msingi (kama vile maana ya maisha) ni suala linalozua mabishano mengi katika jamii za sayansi na falsafa ya sayansi.
Hata hivyo, sayansi inaweza kutupa muktadha fulani na huiweka baadhi ya mipaka ya mazungumzo kuhusu mada kama hizo.

Umuhimu wa kisaikolojia na thamani katika maisha

Sayansi huenda ikashindwa kutuambia nini ni cha thamani maishani, lakini baadhi ya fani zake hugusia maswali yanayohusiana: watafiti katika saikolojia chanya hutafuta sababu zinazoleta hali ya ndani ya kuridhika na maisha. kujihusisha vikamilifu katika shughuli, kufanya mchango zaidi kwa kutumia vipawa vya kibinafsi,
Aina moja ya mfumo wa thamani iliyopendekezwa na wataalamu wa elimunafsia ya jamii, iitwayo kwa upana "Nadharia ya Kupambana na Mambo ya Kutisha", inasema kwamba maana yote ya binadamu inatokana na hofu ya msingi ya kifo, ambapo maadili yanachaguliwa yanapotusaidia kuepukana na kumbukumbu ya kifo.
Sayansi ya niurolojia imetunga nadharia ya malipo, raha na msukumo katika masuala ya kimwili kama shughuli za kupitisha ujumbe za kiniuro. Ikiwa mtu anaamini kwamba maana ya maisha ni kufanya raha ziwe nyingi iwezekanavyo, basi nadharia zinatoa utabiri unaozidi kuongezeka, kuhusu jinsi ya kufanya ili kufanikisha hilo.
Somo la kijamii linapima thamani katika ngazi ya kijamii kwa kubuni nadharia kama vile nadharia ya thamani kanuni, anomi, n.k.

Asili na hali ya maisha ya kibiolojia

Kufanya kazi kwa abayojenesisi hakueleweki kwa ufasaha: nadharia mashuhuri ni pamoja na nadharia ya dunia ya RNA (vitoaji aina sawa katika makao ya RNA) na nadharia ya dunia ya chuma-sulfuri (umetaboli bila Jenetikia). Nadharia ya mabadiliko ya viumbe haijaribu kuelezea asili ya uhai, bali mchakato ambao viumbe tofauti vimepitia katika kipindi chote cha historia kupitia mabadiliko ya ghafla ya kijenitikia na uteuzi wa kiasili Wakati wa mwisho wa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu wa mabadiliko ya viumbe unaotegemea jeni hasa, wanabiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig, miongoni mwa wengine, wanahitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu.
Ingawa wanasayansi wameyachunguza maisha yalivyo duniani, kuyafafanua bayana bado ni changamoto. Kimwili, mtu anaweza kusema maisha "hula entirofi hasi" ambayo walio hai wanapunguza entirofi yao ya ndani kwa gharama ya aina fulani ya nishati inayochukuliwa ndani kutoka mazingira.
Wanabiolojia kwa jumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za kimetaboliki hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu uhai kuendelea kwa vizazi vingi. Kwa kawaida, maumbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za kijenitikia, hivyo huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu marekebisho kupitia mabadiliko ya kimwili. Sifa hizo huongeza nafasi ya kuishi ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo.
Viwakala visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa jumla havitazamwi kama viumbe kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendesha shughuli za kimetaboliki. Pambano hilo ni tatizo, ingawa baadhi ya vimelea na visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi maisha ya kujitegemea.
Astrobiolojia inajihusisha na masomo ya uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe hai katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa vingine visivyo DNA.

Asili na hatima ya ulimwengu

Ingawa dhana ya Mlipuko mkuu ilipozinduliwa mara ya kwanza ilipambana na shaka kwa wingi, shaka iliyochangiwa na uhusiano na imani ya dini ya uumbaji, imekuja kuungwa mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea. Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza kuelezea tu ulimwengu ulivyokuwa mapema sekunde 10 baada ya kutokea. Wanafizikia wengi wamedadisi nini inaweza kuwa imetangulia, na jinsi ulimwengu ulivyoanza. Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko mkuu ulitokea kiajali, na kanuni ya kianthropiki inapozingatiwa, mara nyingi hutafsiriwa kuashiria uwepo wa ulimwengu maridhawa.
Hata hivyo, haijalishi jinsi ulimwengu ulivyokuja kuwepo, hatima ya binadamu katika ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu utaishi muda huo wote - maisha ya kibiolojia hatimaye yatashindwa kujiendeleza.

Maswali ya sayansi kuhusu akili

Hali ya kweli na asili ya fahamu na akili yenyewe pia vinajadiliwa sana katika sayansi. Suala la hiari pia linaonekana kuwa na umuhimu wa msingi. Masuala hayo hupatikana zaidi katika nyanja za sayansi koginitivu, niurolojia na falsafa ya akili, ingawa baadhi ya wanabiolojia wa mabadiliko ya viumbe na wanafizikia wa kinadharia pia wameliashiria sana suala hilo.
.
Mbinu nyingine, kwa vile Mfano wa Rasimu Nyingi, hudai kwamba fahamu inaweza kuelezwa kikamilifu na niurolojia, kupitia utendaji kazi wa ubongo na niuroni zake, hivyo kushikilia ubiolojia wa kihalisia.
Kwa upande mwingine, wanasayansi kama Andrei Linde wanadhani kwamba fahamu, kama nafasi-wakati, huenda ikiwa na ngazi zake za ndani za uhuru, na kwamba maoni ya mtu binafsi yanaweza kuwa halisi kama (au hata kuliko) vifaa tunavyoweza kuvigusa na kuviona.
Nadharia ambazo hazijabainishwa za fahamu na nafasi-wakati zinaelezea kuhusu fahamu katika kuelezea "nafasi ya vipengele vyenye fahamu", mara nyingi zikijumuisha idadi kubwa ya mitazamo ya ziada.
Nadharia za sumakuumeme za fahamu zinatatua tatizo lenye vipengele vingi la fahamu kwa kusema eneo la sumakuumeme linalotokana na ubongo ndilo hasa linalobeba fahamu zoefu. Hata hivyo kuna kutokubaliana kuhusu kutekelezwa kwa nadharia kama hiyo inayohusu utendaji kazi kwingine kwa akili.
Nadharia za akili za kikwontamu hutumia nadharia ya kwontamu kuelezea baadhi ya sifa za akili.
Ikitegemea hoja ya maelezo ya akili yasiyoweza kugusika, baadhi ya watu wamependekeza uwepo wa fahamu ya kikozmiki, wakidai kwamba fahamu kwa kweli ndiyo "msingi wa yote kuwepo". Wanaounga mkono mtazamo huo wanaelezea matukio yasiyo vya kawaida, hasa uwezo wa kuhisi usio wa kawaida na uwezo wa kuyasoma mawazo, kama ushahidi wa uwepo wa fahamu ya juu isiyoeleweka. Katika matumaini ya kuthibitisha uwepo wa mambo hayo yasiyokuwa ya kawaida, wanaelimunafsia wa mambo yasiyo ya kawaida wamefanya majaribio mbalimbali. Uchambuzi unaoangalia mambo yote yaliyopo unaonyesha kuwa idadi ya wenye nguvu zisizo za kawaida (ingawa ndogo sana) kwa ulinganishaji imebaki thabiti. Ingawa baadhi ya wachambuzi wakosoaji wanahisi kuwa somo la elimunafsia isiyo ya kawaida ni sayansi, hawaridhishwi na matokeo ya majaribio yake.
Wanaochunguza mambo haya upya, wanabaki na wasiwasi kwamba matokeo yanayoonekana kuwa na mafanikio huenda yakawa yanatokana na utaratibu mbaya, na watafiti wasiokuwa na mafunzo ya kutosha, au mbinu hafifu.

Mitazamo ya kifalsafa

Mitazamo ya kifalsafa kuhusu maana ya maisha ni itikadi ambazo huelezea kuhusu maisha kupitia suala la maadili au dhana zinazofafanuliwa na binadamu. 

Plato alikuwa mmoja wa wanafalsafa wa mwanzo, na mwenye ushawishi mwingi hadi leo - hasa kwa uhalisia kuhusu uwepo wa viulimwengu. Katika Nadharia ya Maumbo, viulimwengu havipo kimwili, lakini vipo katika maumbo ya kipepo au kimbingu. Katika Jamhuri mazungumzo ya mhusika wa mwalimu wake Sokrates yanaelezea Umbo la Zuri, jambo la kimaadili, hali kamili ya uzuri, hivyo basi kipimo cha ujumla cha haki. Katika falsafa ya Plato, maana ya maisha ni kufikia umbo la juu zaidi la elimu, ambalo ni Umbo la Zuri, ambapo mambo yote mema na ya haki yanatoa umuhimu na thamani. Binadamu wamefungwa na wajibu wa kuyatekeleza mazuri, lakini hakuna yeyote anayeweza kufanikiwa katika harakati hiyo bila fikira.........<ITAENDELEA>>>>>>

Tuesday, December 29, 2015

VIJUE VYUO VIKUU VILIVYO DAR ES SALAAM

1.University of Dar es Salaam 

      Image result for university of dar es salaam
    Map of university of dar es salaam
University of Dar es Salaam 
Public university in Dar es Salaam, Tanzania
The University of Dar es Salaam is a public university in Dar es Salaam, Tanzania. It was established in 1961 as an affiliate college of the University of London. Wikipedia
Address: University of Dar ES Salaam Mlimani, Dar es Salaam
Enrollment: 19,650 (2007)
Founded: July 1, 1970
 
2. Muhimbili University of Health and Allied Sciences 
University in Tanzania
Muhimbili University of Health and Allied Sciences is a public university in Dar es Salaam, Tanzania. Wikipedia
Address: United Nations Rd, Dar es Salaam
Founded: 2007
 
3. Ardhi University 
University in Dar es Salaam, Tanzania
      Image result for ardhi university
    Map of ardhi university

Ardhi University is a public university in Dar es Salaam, Tanzania. It was established 28 March 2007, though it has been offering training for more than 60 years in different status. Wikipedia
Address: Makongo, Dar es Salaam
Founded: 2007
 
 
4. Open University of Tanzania 
University in Dar es Salaam, Tanzania
      Image result for open university of tanzania
    Map of open university of tanzania

The Open University of Tanzania is a distance learning public university in Tanzania. It was established by an Act of Parliament No. 17 of 1992. Wikipedia
Address: Kinondoni, Dar es Salaam
Founded: 1992
 
5. Dar es Salaam University College of Education 
College in Dar es Salaam, Tanzania
 
Image result for duce university
Map of duce university

The Dar es Salaam University College of Education is a constituent college of the University of Dar es Salaam in Tanzania. Wikipedia
Address: Taifa Rd, Dar es Salaam
Founded: 2005
 
6. St. Joseph University In Tanzania 
University in Dar es Salaam, Tanzania
Image result for st joseph university in tanzania
Map of st joseph university in tanzania

St. Joseph University In Tanzania is a private university in Dar es Salaam, Tanzania. Wikipedia
Address: A7, Dar es Salaam
Founded: 2011
 
7.International Medical and Technological University
University in Dar es Salaam, Tanzania
      Image result for international medical and technological university

The International Medical and Technological University is a private university in Dar es Salaam, Tanzania. Wikipedia
Founded: 1997
 
 
8. Hubert Kairuki Memorial University 
University in Dar es Salaam, Tanzania
      Image result for hubert kairuki memorial university
    Map of hubert kairuki memorial university

The Hubert Kairuki Memorial University is a private medical university in Dar es Salaam, Tanzania. It is an accredited university recognized by the government Tanzania through the Tanzania Commission for Universities. Wikipedia
Address: Regent Estate, Dar es Salaam
Enrollment: 506 (2007)
Founded: 1997
 
9. United African University of Tanzania
University in Dar es Salaam, Tanzania · uaut.ac.tz
      Image result for united african university of tanzania

The United African University of Tanzania is a private Christian university in Tanzania. It was founded by the Korea Church Mission and is located in Dar es Salaam. Wikipedia
Founded: 2012

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR