Saturday, November 1, 2014
Msomo ya Dominika ya Kumbukumbu ya Marehemu wote, Jumapili ya Tarehe 02/11/2014
02
November
Jumapili: Kuwakumbuka Marehemu wote.SOMO 1. Hek. 3:1-9
Somo katika Hekima.
Roho zao mwenye haki zimo mikononi mwa Mungu, wala maumivu hayatawagusa. Machoni pa watu walio wajinga walionekana kwamba wamekufa, na kufariki kwao kulidhaniwa kuwa ni hasara yaom na kusafiri kwao kutoka kwetu kuwa ni uharibifu wao; bali wao wenyewe wamo katika Imani....
somo 2. Rum. 6:3-9
Somo katika kitabu cha Warumi.
Hamfahamu ya kuwa sis sote tulibatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Bazi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya........
INJILI.Mt. 25:31-46
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: hapo atakapokuja mwana wa Adamu katika utukufu wake, na Malaika Watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume na Mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wa wake wa kuume, njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme, mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu mkanunywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi ukanivika; nalikuwa mgojwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia, ndipo mwenye haki watakapomjibu, wakisema Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha au una kiu tukakunywesha,? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u Mgojwa, au kifungoni, tukakujia? Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amini nawaambia, Kadri mlivyomtendea mmoja wapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika Moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na Malaika zake; kwa maana, nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, usininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgojwa, na kifungoni, usije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana ni lini tulipokuona wewe una njaa , au una kiu, au u mgeni au u uchi, au mgojwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu akisema, Amini, nawaambia, kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika Adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Ratiba ya Ibada ya Jumapili ya tarehe 02/11/2014
Kigango cha Boko
Misa ya Kwanza- saa 12:15 Mpaka saa 1:45 Asubuhi.Misa ya Pili - saa 2:00 Mpaka saa 3:50 Asubuhi.
Misa ya Tatu - saa 4:00 Mpaka saa 5:30 Asubuhi.
Kigango cha Mt. Rafael Mbweni Malindi
Misa ya Kwanza - saa 1:00 Mpaka saa 2:50 Asubuhi
Misa ya Pili - saa 3:00 Mpaka saa 4:50 Asubuhi.
Kigango cha Mt. Fransisco wa Asizi - Mbweni
Misa ya Kwanza - saa 1:15 mpaka saa 2:50 Asubuhi.
Misa ya pili - saa 3:00 mpaka saa 4:50 asubuhi
Kigango cha Mt. Anthony wa Padua - Mbweni Mpiji
Misa ni saa 3:00 mpaka saa 5:00 asubuhi
masomo ya Sikuku ya Watakatifu Wote 01/11/2014
01
November
JUMAMOSI: Sikuku ya Watakatifu Wote. 2014.SOMO 1. Ufu. 7:2-4, 9-14
Somo katika kitabu cha ufunuo.
Mimi Yohane niliona Malaika mwingine, akipanda kutoka mawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale Malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na Bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.......
2. 1Yoh. 3:1-3
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo Mtakatifu.
INJILI.Mt. 21:33-43
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.
Yesu alipowaona Makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio Maskini wa Roho; Maana ufalme wa Mbinguni ni wao. Heri wenye Huzuni; maana hao watafarijika, Heri wenye upole, Maana hao watarithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa Mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; Kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Friday, October 31, 2014
MAFUNZO YA WALIMU WA WALIMU wa UJASILIAMALI
Mafunzo ya walimu wa walimu
"Training of Trainers" kuhusu ujasiliamali yatatolewa kwa Halmashauri
za VIWAWA za Parokia za BOKO na BUNJU siku ya Tarehe 08/11/2014 kwenye ukumbi
wa Masista wa Karmeli Boko. Mafunzo yamepangwa kuanza saa 2:00 asubuhi. Pamoja
na viogozi hao kijana yoyote mwenye nia na anayependa kuhudhuria anakaribishwa.
Tofauti na mafunzo mengine ya
Ujasilimali ambayo hufundisha mfano: - jinsi ya kuzalisha bidhaa mbalimbali,
mafunzo haya yatalenga katika kumwezesha kijana kutambua na kuzitumia mbinu
zifuatazo: -
- Je unataka kuzifahamu "Sifa 12 za mjasilimali mwenye mafanikio?"
- Je unafahamu "Kanuni saba ambazo humuungoza mjasiliamali?"
- Je unafahamu kuwa "biashara/ huduma/ bidhaa inao mzunguko wa maisha na Ipo misingi ya kubadili biashara/ bidhaa husika iwapo haileti faida yoyote?".
- Je ungependa "kubuni biashara mpya kabisa?"
- Je ungependa kufahamu jinsi ya "Kuchagua bidhaa au huduma gani iwe biashara yako?"
- Jifunze "Mbinu za kuingiza biashara/ bidha/ huduma sokoni"
- Jifunze kuhusu "Vyanzo vya mitaji"
- Jifunze kujiandalia mchanganuo wa biashara yako kwa kutumia "Njia rahisi ya kutayarisha mchanganuo wa biashara"
Hizi ni baadhi ya elimu utakazopata
katika mafunzo haya na pia mengine mengi katika mfululizo wa mafunzo siku
zijazo. Kumbuka Biashara inaishi, hukua na hubadilika, hivyo katika kila
hatua mbinu muafaka zinahitajika ili isife.
Mafunzo haya yamegawanyika kama
ifuatavyo: - 40% nadharia na 60% jinsi ya kutenda. Kijana ukitoka katika
mafunzo haya ya awali utajengwa kuwa mwalimu ambaye utashiriki kuongeza timu ya
walimu wa ujasiliamali. Pia utaweza kubuni biashara yako mwenyewe na jinsi ya
kuiingiza kwenye soko lenye ushindani mkali.
Mwana halmashauri, na kijana USIKOSE
fursa hii adimu kwa gharama nafuu sana Jiandikishe sasa. Kwa mawasiliano piga
simu namba 0713 900 905,0784 799 455, 0765 755 519 na0714 118 788
Mapendo…..
Thursday, October 30, 2014
Semina ya Awali (ujasiriamali na kijana)
Tarehe 08/11/2014, Halmashauri za VIWAWA, Parokia ya Boko na Bunju, Watakuwa na Semina Elekezi ya Ujasiriamali, Itakayofanyikia kwenye ukumbi wa masista Wakarmel Boko
Semina Hii itaanza saa 2:00 Asubuhi, na itaongozwa na Mkufunzi wetu, Mr. Aloyce Dinho, zaidi ya hawa viongozi pia tunawakaribisha vijana wengine wenye uelewa wa elimu ya ujasiriamali au wale ambao tayari wanafanya ujasiriamali.
unaweza kuwasiliana nasi kupitia number hii 0713 900 905. bonyeza hapa endelea kusoma hapa>>>>>>>
Semina Hii itaanza saa 2:00 Asubuhi, na itaongozwa na Mkufunzi wetu, Mr. Aloyce Dinho, zaidi ya hawa viongozi pia tunawakaribisha vijana wengine wenye uelewa wa elimu ya ujasiriamali au wale ambao tayari wanafanya ujasiriamali.
unaweza kuwasiliana nasi kupitia number hii 0713 900 905. bonyeza hapa endelea kusoma hapa>>>>>>>
Saturday, October 18, 2014
Kesho Dominika ya tarehe 19/10/2014, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Misa Takatifu mjini Vatican
Baba
Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI ni kati ya viongozi wakuu wa Kanisa
wanaotarajiwa kuhudhuria katika ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya
kumtangaza Mtumishi wa Mungu Papa Paulo VI, Jumapili, tarehe 19 Oktoba
2014 majira ya asubuhi kwa saa za Ulaya. Itakumbukwa kwamba, Baba
Mtakatifu Benedikto XVI aliteuliwa na Papa Paulo VI kuwa Kardinali.
Hadi
sasa kuna Makardinali wawili ambao bado wako hai, hawa ni wale
walioteuliwa na Papa Paulo VI wakati alipokuwa analiongoza Kanisa. Hawa
ni Kardinali Evaristo Arns na Kardinali wakefield Baum. Haya yamesemwa
na Padre Federico Lombardi Msemaji mkuu wa Vatican, siku ya Ijumaa
alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Vatican.
Hili
litakuwa ni tukio la pili la aina yake kwa Baba Mtakatifu mstaafu
Benedikto XVI kushiriki hadharani katika Ibada zinazoongozwa na Papa
Francisko, tangu alipong'atuka kutoka madarakani.
Maadhimisho ya Siku ya 88 ya Kimissionari Duniani kwa Mwaka 2014
Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Siku ya 88 ya Kimissionari Duniani kwa Mwaka 2014.
Mama
Kanisa tarehe 19 Oktoba 2014 anaadhimisha Siku ya 88 ya Kimissionari
Duniani, iliyoanzishwa kunako mwaka 1926 na Papa Pio wa Kumi na moja na
kuanza kuadhimishwa rasmi hapo mwaka 1927 kama siku ya kukoleza ari moyo
wa kimissionari katika kuwatangazia Watu wa Mataifa Habari Njema ya
Wokovu. Hii ni siku ambayo inaadhimishwa mwezi Oktoba, ambao kimsingi ni
mwezi wa kimissionari.
Baba
Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa maadhimisho ya Siku ya 88 ya
Kimissionari Duniani kwa mwaka 2014 anasema kuna umati mkubwa wa watu
ambao haujabahatika kusikia Habari Njema ya Wokovu, Familia yote ya
Mungu inawajibika kushiriki katika Uinjilishaji kwa kutambua kwamba,
Kanisa limeanzishwa na linatumwa kuwatangazia watu juu ya Ufalme wa
Mungu.
Hii ni siku ambayo waamini wanaalikwa kushiriki
kikamilifu kwa njia ya sala na sadaka yao ili kuonesha mshikamano na
Makanisa machanga duniani kama njia ya kumshukuru Mungu kwa neema
sanjari na kuonesha ile furaha ya ndani. Yesu anawatuma wafuasi wake na
kuwategemeza katika shughuli za kimissionari kama inavyojionesha katika
Maandiko Matakatifu pale alipowatuma wafuasi wake Sabini na wawili,
wakarudi huku wakiwa wamesheheni furaha baada ya kutangaza kuhusu Ufalme
wa Mungu na kuwaandaa watu kukutana na Yesu.
Mitume
wanapoonesha furaha yao, Yesu anawataka wafurahi kwa sababu majina yao
yameandikwa mbinguni na kwamba, wamebahatika kuyaona matendo makuu ya
Mungu yakitendwa mbele ya macho yao! Hii si nguvu ya kutoa pepo wachafu,
bali ile nguvu ya upendo ambao wamekirimiwa na Mwenyezi Mungu. Uzoefu
na mang'amuzi haya yanakuwa ni sababu ya furaha hata kwa Yesu Mwenyewe
kiasi cha kumshukuru Roho Mtakatifu, huku akimtolea sifa Baba yake wa
mbinguni, kwani ile siri kubwa kuhusu Ufalme wa Mungu iliyokuwa
imefichika inajionesha kwa njia ya Yesu Kristo na ushindi wake dhidi ya
shetani.
Hii ni siri ambaye imefunuliwa kwa maskini na
wanyenyekevu wa moyo ambao wamebarikiwa mbele ya Mungu. Hawa ni kama
Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu, Wavuvi kutoka Galilaya na Mitume wote
ambao wamebahatika kushikamana na Yesu wakati alipokuwa anawahubiria
watu Habari Njema ya Wokovu.
Baba Mtakatifu anasema, Yesu
anaonesha ile furaha inayobubujika kutoka katika undani wake kutokana na
ufunuo wa mpango wa Mungu katika kazi ya ukombozi wa mwanadamu,
kielelezo cha hali ya juu kabisa cha upendo wa Mungu kwa mwanadamu kwa
njia ya Yesu Kristo. Hii ndiyo furaha iliyokuwa inabubujika kutoka
moyoni mwa Bikira Maria pale alipomtembelea binamu yake Elizabeti
kumshirikisha kuhusu matendo makuu ya Mungu katika maisha yake.
Hii
ndiyo furaha inayoendelea kububujika katika maisha ya waamini hadi
nyakati hizi, anasema Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa
maadhimisho ya Siku ya themanini na nane ya Kimissionari Duniani na
kuwawezesha waamini kuingia katika maisha ya Fumbo la Utatu Mtakatifu.
Mungu Baba ni chemchemi ya furaha, Yesu Kristo ni kielelezo cha furaha
hii na Roho Mtakatifu ndiye mwezeshaji mkuu, changamoto kwa waamini
kumjifunza na kumwendea Yesu ili aweze kuwafariji na kuwakirimia maisha
ya uzima wa milele, wale wote wanaobahatika kukutana na Yesu.
Wale
wanaokombolewa na Yesu, wanaondolewa dhambi, hofu na "jangwa la maisha
ya kiroho" kwani kwa njia ya Yesu, daima waamini wanaweza kupata na
kuendelea kububujika furaha. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Bikira Maria
pamoja na Mitume wake walioamua kubaki pamoja na Yesu ili kushiriki azma
ya Uinjilishaji, Yesu akawa ni sababu ya furaha yao ya ndani!
Baba
Mtakatifu Francisko anasema ulimwengu mamboleo unakabiliwa na hatari
kubwa ya kumezwa na ulaji wa kupindukia unaojikita katika ubinafsi,
mambo yanayousononesha moyo wa binadamu kwa kutaka furaha za mpito
pamoja na dhamiri mfu. Binadamu anachangamotishwa kujichotea wokovu
ulioletwa na Yesu, wafuasi wake wakiwa wa kwanza kuguswa na upendo wake
ili kuwa kweli ni vyombo vya Injili ya Furaha, ili kushiriki ile furaha
ya uinjilishaji.
Maaskofu wana dhamana ya kwanza kabisa katika
utekelezaji wa mchakato wa Uinjilishaji, kwa kujenga na kuimarisha umoja
wa Kanisa mahalia na kuendeleza utume wa Kimissionari hadi miisho ya
dunia, hasa katika maeneo yaliyoko pembezoni mwa dunia, huko ambako kuna
maskini wanaosubiri kwa hamu kubwa kusikia Habari Njema ya Wokovu.
Upungufu
wa miito ya Kipadre na Kitawa ni kielelezo cha Jumuiya kukosa ile
furaha yenye mvuto na mguso, inayobubujika kwa mwamini kukutana na Yesu
kwa kuwashirikisha pia maskini. Hii ni changamoto kwa Parokia na Vyama
vya Kitume kuonesha ushuhuda wa udugu unaojikita katika upendo wa Yesu
pamoja na kuguswa na shida pamoja na mahangaiko ya maskini na wote
wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii. Pale ambapo kuna furaha ya kweli,
hapo pia kuna ari na moyo wa kutaka kuwashirikisha wengine, hapo ni
mwanzo wa miito mitakatifu. Waamini walei wanahamasishwa pia kushiriki
maisha ya kimissionari, ili kutangaza Injili, lakini wanahitaji majiundo
makini.
Baba Mtakatifu anasema kwamba, Siku ya Kimissionari
Duniani ikuze ndani ya waamini wajibu wa kimaadili wa kushiriki kwa
furaha utume wa kuwatangazia Watu wa Mataifa Habari Njema ya Wokovu, kwa
kuchangia kwa hali na mali, kwa kutambua kwamba, sadaka hii ni sehemu
ya mchakato wa Uinjilishaji wa watu unaobubujika kutoka katika upendo.
Baba
Mtakatifu anawataka waamini katika Makanisa mahalia kutokubali kupokwa
ile furaha ya Uinjilishaji. Anawaalika kujizamisha katika furaha ya
Injili kwa kuirutubisha kwa upendo. Furaha ya mfuasi wa Kristo
inajionesha kwa kukaa na Yesu, mwamini anapotekeleza mapenzi ya Mungu na
anaposhirikisha imani, matumaini na mapendo ya Kiinjili.
Imehaririwa na
Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...