Friday, March 15, 2013

speech ya Pope

Wasifu wa Baba Mtakatifu Francis!



Baba Mtakatifu Francis ni Myesuiti wa kwanza kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Ni Papa wa kwanza katika historia ya Kanisa kutoka nje ya Bara la Ulaya na Papa wa kwanza katika historia ya Kanisa kutoka katika nchi za Amerika ya Kusini, nchi ambazo kwa sasa zina idadi kubwa ya waamini wa Kanisa Katoliki. Kwa mara ya kwanza Jina la Mtakatifu Francis linatumiwa na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Lakini ikumbukwe kwamba, kuna watakatifu wanne wenye majina ya Francis. Hawa ni akina Mtakatifu Francis wa Assisi, Msimamizi wa Italia; Mtakatifu Francis wa Sale, Mwalimu wa Kanisa na Msimamizi wa Waandishi wa Habari; Mtakatifu Francis Xsaveri, Myesuit na Msimamizi wa Wamissionari pamoja na Mtakatifu Francis wa Paulo, Mkaa pweke na mwanzilishi wa Shirika la Ndugu wadogo wa Calabria.

Kardinali Jorge Mario Bergoglio, SJ, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Buenos Aires, Argentina, alizaliwa tarehe 17 Desemba 1936 mjini Buenos Aires. Yeye ni mtoto wa Mzee Mario na Mama Regina Sivori, waliobahatika kupata watoto watano. Katika ujana wake, alisoma na kufuzu kama mtaalam wa kemia, baadaye akaacha kazi hii na kujiunga Seminarini huko Villa Devoto.

Tarehe 11 Machi 1958 alijiunga na malezi ya Kinovisi katika Shirika la Wayesuit akaendelea pia na masomo dunia nchini Cile na kunako mwaka 1963 alirejea tena Buenos Aires na kujipatia shahada ya uzamili kutoka katika Kitivo cha Falsafa, Chuo Kikuu cha San Josè huko San Miguel.

Kati ya mwaka 1964 na mwaka 1965 alikuwa ni Jaalim wa Fasihi Andishi na Saikolojia katika Chuo cha Bikira Maria wa Santa Fe. Kunako mwaka 1966 akafundisha masomo haya kwenye Chuo Kikuu cha Salvatore cha Buenos Aires. Kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 1970, alijiendeleza kwa masomo ya Taalimungu katika Chuo Kikuu cha San Josè kilichoko San Miguel na kujipatia shahada ya uzamili.

Tarehe 13 Desemba 1969 akapewa daraja takatifu la Upadre. Kati ya mwaka 1970 hadi mwaka 1971 alikamilisha hatua ya tatu ya majiundo yake kama Myesuit huko Hispania na tarehe 22 Aprili 1973 akaweka nadhiri za daima. Kati ya mwaka 1972 hadi mwaka 1973 alikuwa ni mlezi wa Wanovisi, Jaalim, Mshauri na Gombera wa Chuo cha Massimo. Tarehe 31 Julai 1973 akateuliwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Argentina kwa upande wa Shirika, utume ambao aliutekeleza kwa muda wa miaka 6. Kati ya Mwaka 1980 hadi mwaka 1986, alikuwa ni Gombera wa Chuo cha Massimo na Paroko wa Parokia ya Patriaki San Josè, Jimboni San Miguel.

Kunako mwaka 1986 alikwenda nchini Ujerumani kumalizia masomo yake katika Shahada ya Uzamivu na wakuu wake wa Shirika wakampatia jukumu la kuwa mkuu wa malezi ya kiroho na muungamishi katika Chuo cha Salvatore.

Tarehe 20 Mei 1992 Papa Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Buenos Aires, akawekwa wakfu kama Askofu tarehe 27 Juni 1992. Tarehe 3 Juni 1997 akateuliwa kuwa Askofu mwandamizi wa Jimbo kuu la Buenos Aires na tarehe 28 Februari 1998 akasimikwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Buenos Aires baada ya kifo cha Kardinali Antonio Quarracino na hivyo kuwa pia ni Mkuu wa Kanisa Katoliki Argentina.

Mwenyeheri Yohane Paulo II akamteuwa na kumsimika kuwa Kardinali kunako tarehe 21 februari 2001. Ameshiriki katika Sinodi ya Maaskofu iliyofanyika kunako mwaka 2001. Akashiriki pia kwenye mkutano wa Makardinali wakati wa uchaguzi wa Papa kati ya tarehe 18 na 19 Aprili 2005. Alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri ya Sinodi ya kumi na moja ya Maaskofu kuanzia tarehe 2 hadi 23 Oktoba 2005.

Mjini Vatican alikuwa ni mjumbe wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri, Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri na Mjumbe wa Sekretarieti ya Sinodi.

Nchini Argentina alikuwa ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Argentina.
Rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Argentina. Alikuwa ni mratibu mkuu wa Mahakama ya Kanisa; Mratibu wa Mahakama ya Jimbo kuu la Buonos Aires. Tangu mwaka 2005 hadi 2011 alikuwa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Argentina.
Ni mwandishi wa Vitabu vifuatavyo:
    1982: Meditaciones para religiosos
    1986: Reflexiones sobre la vida apostólica
    1992: Reflexiones de esperanza
    1998: Diálogos entre Juan Pablo II y Fidel Castro
    2003: Educar: exigencia y pasión
    2004: Ponerse la patria al hombro
    2005: La nación por construir
    2006: Corrupción y pecado
    2006: Sobre la acusación de sí mismo
    2007: El verdadero poder es el servicio

Wednesday, March 13, 2013

Tamasha 2011


 HICHI KILIKUWA KIKOSI CHA TIMU YA KIGANGO CHA BOKO - 2001
NA HII NDIYO ILIKUWA TIMU YA KIGANGO CHA BUNJU KWA MWAKA 2011

Tuesday, March 12, 2013

Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican

Jiografia ya Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican



Wakati huu wa uchaguzi wa Papa Mpya jambo la msingi kukumbuka ni kwamba, Kanisa ni moja, Takatifu, Katoliki, na la Mitume. Makardinali katika mwelekeo wa mawazo yao ya jumla wamebainisha kwamba, wanataka kumchagua Kiongozi mkuu wa Kanisa atakayeliongoza Kanisa la Kristo kama Baba mwenye huruma na mapendo, kielelezo cha umoja na mshikamano wa Kanisa; kiongozi mwenye dhamana ya kulinda na kusimamia kweli za Kiinjili, Maadili na utu wema. Haijalishi mahali anapotoka mtu, jambo la msingi ni kiongozi.

Kwa jumla, kuna Makardinali 115 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wanaoanza mchakato huu kwenye Kikanisa cha Sistina kwa kula kiapo, tafakari ya Neno la Mungu na uchaguzi wa kwanza. Makardinali 60 wanatoka katika nchi za Ulaya, kuna Makardinali 33 kutoka Amerika, Makardinali 11 kutoka Barani Afrika, Asia kuna Makardinali 10 na Oceania kuna Kardinali mmoja. Itakumbukwa kwamba, kwenye Conclave ya Mwaka 2005, Kenya haikuwa na Kardinali, lakini mwaka huu, Kardinali John Njue yupo.

Kuna Makardinali 40 ambao wametekeleza utume wao au bado wanaendelea kufanya shughuli mbali mbali mjini Vatican. Kati ya Makardinali wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura 67 ni wale walioteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.

Wastani wa umri wa Makardinali wanaopiga kura ni kati ya miaka 71. Kardinali Walter Kasper mwenye umri wa miaka 80 ni kati ya wale waliobahatika kuingia katika Conclave wakiwa na umri mkubwa zaidi. Kati ya Makardinali vijana wana umri wa miaka 54 na 56. Kardinali Luis Antonio Tagle ana umri wa miaka 56.

Mwishoni, itakumbukwa kwamba, kundi la Makardinali Maaskofu lina Makardinali 6; Kundi la Makardinali Mapatriaki lina jumla ya Makardinali 4; Kundi la Makardinali Mapadre lina jumla ya Makardinali 153 na Makardinali Mashemasi wako 44. Kuna jumla ya Makardinali 207.

Hatua za mwisho mwisho(PAPA)

Hatua za mwisho mwisho kabla ya Papa Mpya kutokeza hadharani!



Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro unakamilika kwa Kardinali kupata theluji mbili ya kura zote halali zilizopigwa. Baada ya hapo, Dekano wa Makardinali ambaye wakati wa uchaguzi ni kardinali Giovanni Battista Re, atamuuliza Kardinali aliyechaguliwa kama anakubali kisheria kwamba, amechaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baada ya hapo, ataulizwa jina ambalo atalitumia katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Wakati wote huu, Mshehereheshaji mkuu wa Papa ndiye atakayekuwa anachukua rasmi taarifa zinazotolewa na Papa Mteule akisaidiwa na Washereheshaji wengine wawili wanaokuwepo mahali hapo kama Mashahidi. Seehemu hii ya mchakato ikikamilika, hapo karatasi zilizotumika kwa ajili ya kupigia kura zinachomwa na hapo moshi mweupe unatoka kuashiria kwamba Kanisa limempata Papa Mpya.

Papa Mpya ataelekea kwenye "Chumba cha machozi" neno ambalo pengine linaonesha ile hali ya ndani anayokuwa nayo Kardinali baada ya kuambiwa kwamba, amechaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anaporudi kwenye Kikanisa cha Sistina, Injili inayozungumzia Ukulu wa Mtakatifu Petro inasomwa, Makardinali wanasali kwa kitambo kidogo na hapo Makardinali moja baada ya mwingine wanaanza kwenda kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, wakati wote huu, Makardinali na Papa wanaendelea kumshukuru Mungu kwa kuimba utenzi wa shukrani, Te Deum.

Padre Lombardi anasema, Papa Mpya kabla ya kwenda kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kutoa baraka zake kwa mji wa Roma na Ulimwengu kwa ujumla, "Urbi et Orbe" atapitia kwanza kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Paulo kusali kwa kitambi kifupi na baadaye atawasalimia na kuwapatia baraka zake za kitume waamini, mahujaji na wote watakaokuwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Papa mpya ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kusimikwa kwake, siku yoyote inayoonekana inafaa zaidi!

Shirikisha Invia articolo

Monday, March 11, 2013

  1.  JUMATANO TAREHE 13/03/2013
 Kutakuwa na kikao cha dharura cha halmashauri ya VIWAWA Parokia ya Boko Agenda maandalizi ya Hija Bagamoyo- kikao kitafanyika saa kumi na mbili na nusu jioni Parokia Boko....fika bila kukosa
 2.JUMAMOSI TAREHE 16/03/2013
Vijana wote wa Parokia tutashiriki katika Hija ya Vijana wa Jimbo la Dar es salaam itakayofanyikia Bagamoyo.......Usafiri utafika Vigangoni saa moja asubuhi tayari kwa safari...
    
  JUMAPILI TAREHE 17/03/2013
      RATIBA ZA IBADA ZA MISA TAKATIFU
KIGANGO CHA BOKO.
MISA YA KWANZA 12:30-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI     SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI 
MISA YA KWANZA SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 4:00-5:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 2:00-4:00 ASUBUHI.

KIKAO CHA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA

Halmashauri ya WALEI Parokia watakuwa na Kikao mara baada ya Misa ya Pili Saa 4:00 asubuhi kikao kitafanyikia Parokiani Boko wajumbe wote mnatakiwa kufika Bila kukosa. ni siku ya Uchaguzi wa Viongozi wa WALEI ngazi ya Parokia.

....Wasilisha Mchango wako wa Hija ya Bagamoyo kwa Mhazini wa Jumuiya yako au Kigango chako Kabla ya Tarehe 09/03/2013..........

anza maandalizi ya ibada ya matawi don bosco tarehe 24/03/2013 mchango ni tshs 3500

Saturday, March 9, 2013

HISTORIA YA JIMBO LA MOROGORO

Jimbo Katoliki la Morogoro Historia
Historia Fupi ya Jimbo
-         Jimbo la Morogoro lilizaliwa Machi 25, 1953 na Mhasham Bernard Hilhorst alikuwa askofu wake wa kwanza.
-         Hata hivyo, historia ya Jimbo la Morogoro inaanza karne ya 19 katika miaka ya 1860. Mapema mwaka 1858 Askofu Amandus R. Maupoint wa Jimbo Katoliki la Mtakatifu Denis, Reunion alifanya makao yake Kisiwani Unguja. Miaka miwili baadaye Wamisionari wengine walikuja Unguja kufanya uinjilishaji.   Baada ya miaka michache ilionekana ilifaa kazi ya uinjilishaji Unguja ikabidhiwe kwa Shirika la Kidini lenye uzoefu. Shirika la Mapadri wa Roho Mtakatifu walikabidhiwa jukumu hilo.
-   Novemba 12, 1862  Unguja  ilipandishwa hadhi toka “Mission Territory”  na kuwa “Apostolic Prefecture of Zanguebar.”  Unguja  ikapata Msimamizi wa Kitume chini ya  Mamlaka ya Askofu Maupoint.
-         Juni 16, 1863  Mapadri  Anthony Horner na Edward Baur na Mabradha  Celestine na Felician wa Shirika la Roho Mtakatifu waliingia Unguja na  Baadaye mwaka 1868 Wamissionari  hao waliongozwa na Padre Horner   walifika Bagamoyo mara ya kwanza Machi 4, 1868.
-         “Apostolic Prefecture of Zangueber, kama eneo la Kitume lilivyojulikana siku hizo, lilikuwa ni pamoja na Kisiwa cha Unguja na ukanda wa mashariki kuanzia Guardafui hadi Cap Delgado, yaani eneo lote la Afrika ya Mashariki.
-         “Prefecture”  hiyo iligawanywa katika sehemu mbili kuu Wamisionari wa Afrika yaani “White Fathers”walipoingia Unguja April 29, 1878. Hivyo, sehemu iliyojulikana kama ya Maziwa Makuu ambayo ilikuwa ni pamoja na Nyanza ambayo kwa sasa ni Jimbo Kuu la Mwanza, Musoma, Shinyanga na Geita; Tanganyika, ambayo ni Majimbo ya Kigoma, Sumbawanga na Mbeya na Congo ilikabidhiwa kwa Mapadri hao wapya, Wamisionari wa Afrika. Na sehemu iliyobaki ilikuwa bado chini ya Shirika la Roho Mtakatifu.
-         Mwaka 1887 sehemu ya “Prefecture” ambayo sasa ilipata hadhi ya kuitwa “Vacariate” of  “Zanguebar” nayo ikagawanywa katika sehemu kuu tatu:
(a)   Zanguebar Kaskazini na Nairobi. Hii ilijumlisha Mombasa.
(b)  Zanguebar Kusimi, yaani Kilwa na Mzizima au Dar es Salaam.
(c)  Zanguebar Kati, ambayo mwaka 1906 iliitwa Vicariat ya Bagamoyo.
-         Zanguebar Kusini ilikabidhiwa kwa Wamisionari Wabenediktini. Ilikuwa na hadhi ya “Prefecture.”
-         Mwaka 1910 Vikariat ya Bagamoyo iligawanywa tena katika sehemu mbili, yaani Vikariat ya Kilimajaro na Vikariat ya Bagamoyo. Zote zilikuwa chini ya Shirika la Roho Mtakatifu.
-         Mwaka 1934 Vikariat ya Dodoma  ilizaliwa, sehemu ilimegwa toka Vikariat ya Dar es Salaam na Vikariat ya Iringa, na sehemu nyingine ilimegwa toka Vikariat ya Bagamoyo.
-         Mwaka 1950 Vikariat ya Bagamoyo ikamegwa na kuunda Vikariat ya Tanga na miaka mitatu baadaye, yaani Machi 25, 1953 wakati Majimbo yalipoundwa Tanganyika, Vikariati ya Bagamoyo iliyobakia ikapata hadhi ya Jimbo na kuwa Jimbo la Morogoro wakati Dar es salaam ikainuliwa na kupata hadhi ya kuwa Jimbo Kuu la Dar es salaam.  
Maaskofu wa Morogoro  
-         Tangu kuanzishwa kwake kama Vikariat ya
Bagamoyo mwaka 1906, wafuatao ndio Maaskofu Wake:  
Askofu Raoul De Courmont (1883 - 1896)
Askofu Emille Allgeyer (1897 - 1906)
Askofu F.X.Vought (1906 – 1923)  
Askofu B.Wilson (1924 – 1933)  
Askofu Bernard Hilhorst (1934 – 1954)
Askofu Herman V.Elswijk (1954 – 1967)  
Askofu Adrian Mkoba (1967 – 1992)  
Askofu Telesphor Mkude (1992 sasa)
-         Mhasham Adrian Mkoba ndiye Askofu wa kwanza  Mzalendo wa Morogoro.
    

  Hali ya Kijiografia  
-         Jimbo Katoliki la Morogoro limeundwa na eneo lipatalo kilomita za mraba 43,380 kusini mashariki mwa Jamhuri ya Tanzania. Jimbo la Morogoro limeundwa kutokana na Wilaya za Serikali tano, yaani Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Kilosa, Mvomero, na Bagamoyo. Wilaya ya Bagamoyo ni sehemu ya Mkoa wa Pwani Kiserikali, wakati Wilaya nne zilizobaki zipo katika Mkoa wa Morogoro.
-         Makao Makuu ya Mkoa wa Morogoro yapo katika Manispaaa ya Morogoro. Vile vile katika Manispaa hii yanapatikana Makao Makuu ya Jimbo la Morogoro, Kanisa Kuu la Jimbo, na Makao ya Askofu wa Jimbo.  
Wakazi wa Jimbo  
-        Jimbo la Morogoro lina wakazi wapatao 1,559,271.  Kati ya hao wakatoliki ni 638,591.
-         Ni asilimia ishirini (20%) tu ya wakazi wa Jimbo la Morogoro wanaishi mijini, wakati asilimia kubwa, yaani 80%, wanaishi vijijini.
-  Makabila asilia yanayopatikana Jimboni Morogoro ni Waluguru, Wanguu, Wakutu, Wazigua,  Wakami, Wakaguru, Wavidunda, Wasagara, Wakwavi, Wakwere, Wazaramo na Wadoe,
-         Mbali ya makabila haya asilia, Jimbo la Morogoro lina wahamiaji vile vile. Makundi haya ya wahamiaji wengi wao ni Wachaga, Wamasai, Wangoni na Wagogo.
-         Kila kabila lina lugha yake ya asili. Hata hivyo, Kiswahili kinatumika katika sehemu zote katika Jimbo la Morogoro

MASHIRIKA YALIYOPO JIMBO LA MOROGORO
Vito mbalimbali katika taji la dhahabu ambalo Kristo amempamba Bibiarusi wake. Au fungu zuri la maua ya kila rangi. Ni mifano miwili iliyotumika kuelezea wingi wa mashirika ya kitawa ndani ya Kanisa Katoliki. Jimbo la Morogoro ni mojawapo kati ya yale yanayofurahia zaidi neema kubwa namna hiyo.
Tukirudi nyuma hadi karne ya XIX , tunakuta kwamba watawa wa Roho Mtakatifu (Holy Ghost Fathers) ndio waanzilishi wenyewe wa Kanisa nchini, wakitokea Zanzibar na Bagamoyo, na kufuatwa muda si mrefu baadaye na masista kutoka kisiwa cha Réunion (Filles de Marie) Hivyo tangu awali watawa wamekuwa mstari wa mbele sio tu katika maisha ya Kiroho, bali pia katika umisionari.
Mwanzo mgumu: kwa miaka mingi mashirika hayo yaliinjilisha wakistahimili tabu na hari za mchana, mpaka watawa wengine hasa wananchi, tunda la kazi yao, wakaja kuwaunga mkono kwa saa tofautitofauti.
Masista wengi wa nchi nzima wanafahamu sana jimbo hili kwa sababu waliwahi kusoma Bigwa, katika sekondari iliyoanzishwa kwa ajili yao na Umoja wa Mama Wakuu Tanzania (ambao kwa sasa unakamilisha ujenzi wa kituo kingine cha malezi ya pamoja si mbali na shule hiyo).
Hatua mpya ya uwepo wa mashirika jimboni ilipigwa pale ambapo Wasalvatoriani kisha kupatana na mashirika mengine walichagua Morogoro kama mahali pa kujenga seminari kuu ya kitawa ambayo kwa sasa ni Taasisi ya Falsafa na Tauhidi (wengine wanafikiria kuigeuza tena iwe Chuo Kikuu chenye vitivo mbalimbali). Hayati Askofu Adriani Mkoba alifungua milango ya jimbo kulipokea kila shirika litakalohitaji watawa wake wasomee huko. Tangu hapo ujenzi na malezi havijakoma katika eneo la mlima Kola, kwenye barabara ya Dar es Salaam. Yeyote anayepita anajionea maendeleo hayo na kuzungumzia aina hiyo ya Vatikano chini ya milima ya Uluguru.
Mvuto wa taasisi hiyo ndio sababu kuu ya mashirika kumiminika Morogoro miaka ya mwisho; lakini ukianza kuelekea Dodoma, kwenye eneo la Kihonda unakuta vilevile mashirika mengi, ingawa majengo yao yamefichikafichika kati ya nyumba za wananchi.
Kwa jumla sasa hivi jimbo lina mashirika zaidi ya 30 ya kila aina: ya wanaume na ya wanawake, ya kikleri na ya kilei, ya maisha ya wakfu na ya maisha ya kitume, ya kipapa na ya kijimbo. Inakosekana bado monasteri ya maisha ya sala tu, ingawa Askofu Telesphor Mkude ana hamu nayo.
Mhashamu akiona kwa furaha kubwa ongezeko hilo ambalo linaendelea haraka, mwanzoni mwa Jubilei kuu ya mwaka 2000, pamoja na kumteua kwa mara ya kwanza makamu wake maalumu kwa maisha ya wakfu aliamua kuunganisha mashirika hayo yote katika ASSICAL (Association of Institutes of Consecrated and Apostolic Life – Morogoro Diocese) ili yaweze kufahamiana na kubadilishana mawazo, mang’amuzi, matarajio na mipango hasa upande wa malezi na wa utume.
Tangu hapo utume huo unazidi kuimarika kwa njia ya mikutano na adhimisho la pamoja la sikukuu ya watawa iliyoanzishwa na Papa Yohane Paulo II kwenye tarehe 2 Februari ya kila mwaka. Kwa kweli ni tukio la kufurahisha kuona mamia ya watawa wa mabara karibu yote kushangilia miito yao mbalimbali kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Lakini siku moja haiundi mwaka. Kuna siku nyingine 364 ambazo ni nafasi ya kila mtu kumshukuru Mungu kimatendo kwa karama aliyomjalia. Uaminifu wa kila sasa ndio unaothibitisha kwamba neema inapokewa kwa mikono miwili badala ya kuchezewa. La sivyo adhimisho halina maana. Changamoto hiyo ipo daima mbele ya kila mmoja na ya kila jumuia, kwa sababu maisha ya kitawa ni ya kulenga utakatifu pamoja na wengine, sio kibinafsi.
Mbali ya utakatifu, mashirika yanalenga kutoa mchango katika Kanisa na katika jamii, kila moja kadiri ya karama yake. Ingawa nguvu nyingi za mashirika mbalimbali yaliyohamia jimboni kwa ajili ya malezi zinaishia katika kazi hiyo ya msingi, tunaweza kusema nia ya kufanya kitu hata nje ya nyumba ipo. Kadiri ushirikiano unavyostawi, njia zinaonekana, kwa sababu penye nia pana njia.
Mahitaji ya jimbo hasa ni mengi, kama kawaida. Hivyo mapadri na walei wanatazamia sana kufaidika na uwepo wa umati huo wa waamini wenzao waliojitoa kabisa kwa maisha ya wakfu na ya kitume. Baadhi ya mashirika yana nyumba zisizo za malezi, nazo ndizo zinazoitikia zaidi mahitaji hayo. Kwa namna ya pekee Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro, ambao ndio wengi, wanahudumia parokia, shule na zahanati nyingi jimboni kote.
Mungu atujalie sisi sote kushika kwa unyenyenyeku nafasi aliyotupangia katika kufikisha watu kwenye uzima wa milele.  

1. MASHIRIKA YA MAISHA YA WAKFU

 

1.1. Mashirika ya Kitawa

 

1.1.1. Ya Kiume

 
1.      Ndugu Wafransisko Wakonventuali – SLP 932 – Morogoro
Simu: +023/0784594072 – Barua pepe: krzcie@yahoo.com – Tovuti: www.ofmconv.org

2.      Ndugu Wafransisko Wakapuchini – SLP 900 – Morogoro
Simu: +023/2603204 – Barua pepe: kolafriars@yahoo.comTovuti: www.ofmcap.org

3.      Ndugu Waagustino – SLP 1947 – Morogoro
Simu: +023/2604773 – Barua pepe: osamorogoro@yahoo.comTovuti:

4.      Wakarmeli OCD – SLP 363 – Morogoro
Simu: +023/2603800 – Barua pepe: ocdtzmission@yahoo.com – Tovuti:

5.      Shirika la Roho Mtakatifu – SLP 16 – Bagamoyo
Simu: +023/2440063 – Barua pepe: eap@habari.co.tzTovuti

6.      Wamisionari wa Mt. Francis wa Sales – SLP 12 – Morogoro
Simu: +023/2600036 – Barua pepe: msfsmoro@africaonline.co.tz – Tovuti: www.fransalians.com
7.      Shirika la Madonda Matakatifu (Wastigmatini) – SLP 2213 – Morogoro
Simu: +023/2603523 – Barua pepe: stigmatines@morogoro.netTovuti: www.stigmatines.com

8.      Wamisionari Wana wa Moyo Safi wa Maria (Waklareti) – SLP 427 – Morogoro
Simu: +023/2600429 – Barua pepe: cmfmorobarbastro@yahoo.com – Tovuti: www.claret.org
 
9.   Wasalesiani wa Don Bosco – S.L.P. 4045 – Morogoro – Simu: +0764–854602 – Barua pepe:   – Tovuti:
 
10. Wasalvatoriani – SLP 1878 – Morogoro
Simu: +023/2600897 – Barua pepe: sdsschol@go2.pl – Tovuti: http://www.sds–ch.ch/africa
 
11. Wamisionari wa Consolata – SLP 769 – Morogoro
Simu: +023/2603563 – Barua pepe: allasemi@morogoro.netTovuti: http://www.consolata.org
 
12. Shirika la Misheni (Wavinsenti) – SLP 6051 – Morogoro
Simu: +023/2600029 – Barua pepe: depaulmoro04@yahoo.com – Tovuti:

13. Mabradha wa Elimu ya Kikristo wa Mt. Gabrieli (Wamontfort) – SLP 1124 – Morogoro
Simu: +023/2602204 – Barua pepe: montmoro@africaonline.co.tz – Tovuti:
 
 
1.1.2. Ya Kike
 
1.      Mabinti wa Maria (wa St. Denis)– SLP 230 – Bagamoyo
Simu: 023/2440417 – Barua pepe: dmdestdenistan@yahoo.fr – Tovuti:
2.      Masista Wamisionari wa Damu Takatifu – SLP 865 – Morogoro
Simu: +023/2604655 – Barua pepe: – Tovuti:

3.      Shirika la Moyo Safi wa Maria (wa Morogoro) – SLP 1049 – Morogoro

Simu: +023/2603591/2604314 – Barua pepe: mgololesisters@intafrica.com – Tovuti:
4.      Masista wa Msalaba Mtakatifu (wa Chavonod)– SLP 1677 – Morogoro
Simu: +023/2603328 – Barua pepe: holycross@africaonline.co.tz – Tovuti:

5.      Masista Watersiari Wakapuchini wa Familia Takatifu – SLP 1989 – Morogoro
Simu: +023/2604845 – Barua pepe: htctanz@hotmail.comTovuti
:
6.      Masista wa Mt. Anna (wa Luzern) – SLP 1807 – Morogoro
Simu: +023/2601550 – Barua pepe: stannsmoro@africaonline.co.tzTovuti:

7.      Masista Wakolejina wa Familia Takatifu – SLP 945 – Morogoro
Simu: +023/2600424 – Barua pepe: collemoro@hotmail.com – Tovuti:

8.      Masista wa Maria Imakulata (wa Krishnagar) – SLP 2028 – Morogoro
Simu: +023/2604066 – Barua pepe: smimoro@africaonline.co.tzTovuti:

9.      Masista wa Mama wa Karmeli – SLP 1302 – Morogoro
Simu: +023/2600359 – Barua pepe: – Tovuti:

10. Masista wa Mt. Gemma – SLP 304 – Morogoro
Simu: +0784/457358 – Barua pepe: – Tovuti:
 
11. Masista Waursula wa Yesu Mteswa – SLP 1048 – Morogoro
Simu: +0756/937297 – Barua pepe: – Tovuti:

12. Masista wa Sakramenti Kuu – SLP 2135 – Morogoro
Simu: +023/2602902 – Barua pepe: – Tovuti:

13. Mabinti wa Mt. Fransisko wa Sales – SLP 640 – Morogoro
Simu: +023/2600900 – Barua pepe: dsfstanzania@rediffmail.comTovuti:

14. Masista wa Maria Imakulata (wa Wroclaw) – SLP 1878 – Morogoro
Simu: +0787/759496 – Barua pepe: – Tovuti:

15. Masista wa Mt. Yosefu (wa Annecy) – SLP 58 – Dumila
Simu: +0745/214343 – Barua pepe: agnesadampukulam@yahoo.com – Tovuti:
 
16. Masista wa Mt. Yosefu (wa Chambery) – SLP 135 – Mikumi
Simu: +0787/710338 – Barua pepe: – Tovuti: www.csjchambery.org
 
17. Masista wa Bikira Maria Malkia wa Mitume – SLP 1925 – Morogoro
Simu: +023/2604165 – Barua pepe: – Tovuti:
 
18. Masista wa Mt. Anna (wa Bangalore) – SLP 363 – Morogoro
Simu: +023/603800 – Barua pepe: – Tovuti:

19. Masista Waabuduo Damu ya Kristo – SLP 6508 – Morogoro
Simu: – Barua pepe: – Tovuti:
 
20. Dada Wadogo wa Mt. Fransisko – SLP 1878 – Morogoro
Simu: +0787/759496 – Barua pepe: – Tovuti:
 
21. Masista Wabenedikto Waafrika wa Mt. Agnes – SLP 6015 – Morogoro
Simu: +0784/464024 – Barua pepe: mlowevicky@yahoo.com – Tovuti:
 
22. Masista wa Mt. Karolo Borromeo – SLP 1232 – Morogoro
Simu: +0732/931181 – Barua pepe: – Tovuti:
 
23. Masista Warosmini wa Maongozi – SLP 133 – Morogoro
Simu: +0787/024621 – Barua pepe: – Tovuti:

24. Masista wa Maryknoll – SLP  – Morogoro
Simu: – Barua pepe: – Tovuti:
 
25. Masista Wafransisko wa Upendo – S.L.P. 6083 – Morogoro
Simu: – Barua pepe: – Tovuti:
 
 
 

1.2. Mashirika ya Kilimwengu

 
1.2.1. La Kiume
 
1.      Mapadri wa Shirika la Kilimwengu katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 640 – Morogoro
Simu: +023/2603340 – Barua pepe: – Tovuti:
 
 
1.2.2. Ya Kike
 
1.      Unitas kwa Afrika – SLP 1003 – Morogoro
Simu: +023/2600138 – Barua pepe: – Tovuti:
2.      Masista wa Grail – SLP 6090 – Morogoro
Simu: +023/2613690 – Barua pepe: – Tovuti:
 
 
 

2. MASHIRIKA YA MAISHA YA KITUME

 

2.1. Ya Kiume

 
1.      Wamisionari wa Damu Azizi – SLP 1925 – Morogoro
Simu: +023/2604165 – Barua pepe: stgascoll @yahoo.com – Tovuti: www.cpps–preciousblood.org

2.      Jumuia ya Mapadri katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 1935 – Morogoro
Simu: +023/2601353 – Barua pepe: – Tovuti:
 
 
2.2. La Kike
 
1.      Jumuia ya Masista katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 6038 – Morogoro
Simu: +023/2601764 – Barua pepe: – Tovuti:
 
 
 
3. TAASISI ZA MALEZI YA PAMOJA KATI YA MASHIRIKA YA KIKE
 
1.      Sekondari ya Masista ya Bigwa – SLP 369 – Morogoro
Simu: +023/2603066 – Barua pepe: bigwasrs@yahoo.com – Tovuti:

2.      Kituo cha Malezi ya Masista cha Kola – SLP 913 – Morogoro
Simu: +023/2600658 – Barua pepe: tcastanzania@hotmail.com – Tovuti:
 
 
 
4. CHAMA (CHA WANAUME NA WANAWAKE)
 
1.      Ndugu Wadogo wa Afrika – SLP 6083 – Morogoro
Simu: – Barua pepe: unwa@unwa.tk Tovuti: www.unwa.tk
 


NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR