Thursday, August 16, 2012

SHUKRANI ZA TAMASHA

Tunamshukuru Mungu kwa kutujalia amani na upendo kipindi chote cha Tamasha la Vijana Parokia ya Boko.
   Pia shukrani zetu za dhati ni kwa Paroko wetu Padre Majeta walezi wetu Padre Dismas, sister Sabina na Fratel Paul na kwa upande wa walei tunawashukuru Baraza la walei parokia pamoja na halmashauri yake yote,Tunawashukuru sana.
  mwisho ni kwa vijana wote walioshiriki na hongera sana kwa timu ya kigango cha Mbweni walioweza kuchukua kombe la mpira wa miguu na Kigango cha Boko waliweza kuchukua kikombe cha mpira wa netball.

Saturday, August 4, 2012

MAJETA CUP

                               hatimaye Vikombe vipo mezani vinawasubiri washindi

teheee teheee Amini sasa



this iz it

Paroko wa Parokia ya Boko Padre Aldolph I.L. Majeta, CPPS akiwa na vikombe vya washindi wa ligi ya parokia ya boko kwa netball na football kombe hili litatolewa jumapili kwenye kilele cha Tamasha la vijana na sikuku ya somo wa parokia yetu Mwenye Heri Isidori Bakanja.

Friday, July 20, 2012

FURAHA%@!!!!!!

    VIWAWA kigango cha Bunju wakiwa na mlezi wa VIWAWA Parokia ya Boko Fratel Paul

Wednesday, July 18, 2012

KUTOKA VIWANJANI
Jana zilichezwa mechi za  ligi ya Parokia ya Boko maarufu kama Majeta cup, mechi ambayo ilikuwa na msisimko mkubwa ilikuwa kati ya Bunju na Mbweni iliyochezwa katika uwanja wa Mbweni, majigambo yalikuwa mengi kabla ya mechi ,mvuto mkubwa ukiwa kwa makocha wa timu hizo ndg James Nkii kocha wa timu ya Bunju, na ndg Fabian Masanja kocha wa timu ya Mbweni. mpira ulikiwa upo sawa kwa timu zote mpaka wakati wa mapumziko timu hizi zilikuwa hazijafungana, kipindi cha pili kilianza kwa nguvu sana, huku kila timu ikifanya mabadiliko ambayo kwa upande wa mbweni, yalizaa matunda kwani walipata magoli wawili ya haraka, dakika chache kabla mpira kuisha bunju nao waliamkaa na kupata goli moja la kufutia machozi mwisho wa mpira matokeo yalikuwa Mbweni 2 na Bunju 1

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR