Tuesday, July 9, 2013

KILA MWENYE PUMZI AMSIFU BWANA

  Nani wa msifu Bwana na vipi? Imeandikwa, Zaburi 150:1-6 . Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika anga la uweza wake msifuni katika matendo yake makuu msifuni kwa kadiri ya ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu msifuni kwa kinanda na kinubi; msifuni kwa matari na kucheza msifuni kwa sese na filimbi. Msifuni kwa matoazi yaliyayo msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. 

Sunday, July 7, 2013

MATOKEO YA MECHI ZA LEO 07/07/13



Matokeo ya mechi ya Kundi B tarehe 07/07/2013



Kigango cha Mt.Maria Del Mathias 3 Kigango cha Mt.Raphael Mbweni Malindi 0



MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI A
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint
Damu Takatifu Boko11005 2 3
Mt.Gasper Boko21 1045 3
Mbweni101002 0


MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI B
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint
MARIA DEL MATHIAS210163 4
MT. RAPHAEL211023 3
ANTHONY WA PADUA211135 1

Wednesday, July 3, 2013

picture za ziara karatu

 Mlezi wetu akiwa amepumzika hapa ni korogwe.
 Hapa ni karatu tunapata kitu cha dinner then tukapumzike kidogo tuendelee na safari
 kumekucha tena tupo karatu tayari kwa safari ya kuelekea Mbulu na hii ni asubuhi
 tukiwa bado karatu hapa tunaelekea Parokia ya Endabashi na tulikaa kwa muda hapa
 Paroko wa endabashi Padre John Almasi akisalimia na Mlezi wetu Padre Ngowi
 Paroko wa endbashi akisalimiana na Mwenyekiti wa VIWAWA Parokia ya Boko
 Hapa ndipo tamko la vijiji vya ujamaa lilipo tolewa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere
 Nyumba ya asili ya wairaq waliitumia wakati wa vita vyao na wamasai


uzuri wa endabashi

Monday, June 24, 2013

UNAZIJUA NGUVU ZAKO?

UMOJA WA VIJANA WAKATOLIKI PAROKIA YA BOKO JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM.
ZIARA YA UINJILISHAJI PAROKIA YA DAUDI JIMBO LA MBULU MKOANI MANYARA 26-30/06/13

Kijana ni mtu wa kike au wa kiume mwenye umri kati ya miaka 18 na 35.
Biblia inasema nini juu ya kijana?
Biblia imenena mambo mengi juu ya kijana, na baadhi ya hayo ni kuwa fahari ya kijana ipo katika nguvu zake (Mithali 20:29). Kijana ana nguvu nyingi, neno la Mungu linakaa ndani yake na kisha amemshinda shetani(1Yohana 2:14b).

Yohana anawaandikia vijana akisema wana nguvu nyingi, pili neno la Mungu linakaa ndani yao na kisha wamemshinda shetani. Nguvu yaweza kuwa ya kiroho au ya kimwili, maana zote ni za muhimu na mara nyingine hutegemeana katika utendaji.
Nguvu moja ikikosekana hujitokeza upungufu unaoweza kupelekea uharibifu kama vile mtu kurudi nyuma kwa sababu ya majaribu. Nguvu ya kimwili ya mtu wa Mungu ikitumika kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu, yaweza kupelekea mtu kuwa na nguvu ya kiroho iletayo ushindi juu ya hila na mitego ya yule mwovu.Hapa ina maana kuwa, kwa mtu wa Mungu ukiwa na nguvu ya kimwili na unaongozwa na Roho wa Mungu utamtumikia Mungu pasipo ulegevu, tofauti na mzee ambaye anaweza kuhitaji kufanya jambo lakini nguvu ya kwenda kufanya hana, hilo nalo Mhubiri aliliona na kumhamasisha kijana kutumika akiwa bado anazo nguvu. Mhubiri12:1 ”Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya…“ Yohana anawaandikia vijana akionyesha sifa za aina ya vijana aliokuwa akiwalenga. Anatazamia kwamba kijana akiitumia nguvu hiyo kama ilivyokusudiwa na Mungu, na kulisoma neno, kuomba kwa bidii zake zote, matokeo yake atakuwa na hazina tele ya neno ndani mwake, na kisha atamshinda shetani, maana anazo nguvu za kiroho na za kimwili. Kijana wa aina hii hana hofu maana hata shetani akija kwa sura gani au akitumia mazingira gani, haogopi maana silaha alizo nazo (Neno) ni tishio kwa adui. Mungu anawatafuta vijana kama hao wabebao silaha hiyo ya Bwana , nyakati zote, kila mahali na kwa bidii. ”..Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu“(I Yohana 2:14b).
Biblia inasema kijana akilitii Neno la Mungu na kulifuata litasafisha njia yake. Litamkamilisha kwa kiwango anachotaka Mungu, kwa makusudi ya Mungu na kwa utukufu wa Mungu. Kwahiyo ili kijana aweze kuishi maisha matakatifu, yenye ushindi tele na yanayomtukuza Mungu yampasa kuisafisha njia yake kwa kutii, akilifuata neno la Mungu. Zab.119.9 ”Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.“
Kijana, kufanikiwa kuisafisha njia yako kutategemeana na wewe mwenyewe utakavyotumia nguvu zako. Yakupasa kuelekeza nguvu zako katika maombi, kujisomea Neno la Mungu, hii ni pamoja na kulitafakari na kulitendea kazi. Kwa kufanya hivyo utapata nafasi nzuri ya kumsikiliza Mungu na kujua ni nini mpango na makusudi yake kwako. Kijana hupaswi kulala usingizi tangu jioni hadi asubuhi na tangu January hadi Desemba, huo ni msiba wa kutosha kwa kijana maana Biblia inasema mtu wa aina hiyo atapata umaskini wa kumtosha. Si vema kijana kuzagaa, ukikutwa na adui ukiwa umezagaa atakutumikisha katika matakwa yake. Ni muhimu sana kijana kuwa na mikakati na kuiombea ili kupata uongozi wa Roho Mtakatifu. Mungu anajali sana kijana kuwa na mkakati. Mfano mzuri ni namna alivyomwandaa Yoshua kushika nafasi ya Musa. Awali ya yote alimhakikishia uwepo wake pamoja na kijana huyo, na akamwahidi kutomwacha wala kumpungukia kabisa: ”Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako…sitakupungukia wala sitakuacha.“ (Yoshua 1. 5).
Hapa Mungu anamhakikishia Yoshua kuwa, hata kutokee tatizo kubwa kiasi gani, hata vitisho viwe vikubwa namna gani, hata ainuke nani, asingeweza kuzuia wala kukwamisha kusudi la Mungu katika huduma aliyokuwa anakabidhiwa na Mungu, ya kuwafikisha Waisraeli nchi ya Kanaani. Hali kadhalika wewe kijana, yumkini bado unawategemea wazazi au ndugu, lakini kwakuwa hawakubaliani na Imani yako labda wamekutenga, hawataki kukupa huduma, hata masomoni unatishiwa kufukuzwa kwasababu huna karo; yumkini umeoa au umeolewa na huyo mume au mkeo anakutesa kwa ajili ya Imani yako; kazini unanyanyaswa na mkubwa wako wa kazi au wafanyakazi wenzio, halikadhalika kwenye biashara zako wanakutesa kwa njia mbalimbali. Katika hali yoyote ile, jambo la muhimu uwe na uhakika kwamba Mungu yupo pamoja na wewe na kwamba hatakuacha wala hatakupungukia. Hivyo usikate tamaa, azimia kutomwacha Mungu kabisa, simama katika haki na ahadi za Mungu, utaona ushindi mkubwa.
Baada ya Mungu kutoa uhakika juu ya uwepo wake kwa kijana huyo Yoshua, alimpa mikakati ya namna atakavyoweza kufikia lengo ambalo lilikuwa kuwafikisha Waisraeli katika nchi ya ahadi, Kanaani. Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo:

1. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi….
Mungu hapendezwi na uvivu, alitaka Yoshua awe hodari tu na ushujaa mwingi na siyo mtu wa kujihurumia hurumia bali awe mwepesi wa kwenda anakotakiwa, kutekeleza majukumu ambayo Mungu angempa inavyotakiwa, kwa wakati unaotakiwa, na pasipo hofu. Huo ndiyo ushujaa.

2. ...uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume au wa kushoto.(Yosh. 1.7).
Mungu anamwambia Yoshua, aangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuwa ameamriwa na Musa mtumishi wake Mungu. Swala kuu hapa ni utii wa neno la Mungu. Kwamba kijana hatarajiwi kuwa msikilizaji tu wa Neno la Mungu na kuendelea na maisha ya kidunia. Kijana anahitajika kuwa msikiaji na mtendaji/mtekelezaji wa maagizo ya Mungu ndani ya Neno.
Mungu anasisitiza katika mstari wa nane kuhusu kutafakari Neno. Mungu alimtaka Yoshua, kuhakikisha siku zote za maisha yake anafanya Neno la Mungu kuwa sehemu ya maisha yake. Alimtaka akiwaza awaze (atafakari) Neno mchana na usiku, maongezi yake yawe na msingi katika Neno. Kuhusu kutendea kazi Neno, Mungu alimwambia Yoshua aangalie kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo (ndani ya torati/Neno.
”Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo…."(Yoshua 1:8).
Kwa maana hiyo, iwe usiku iwe mchana kijana saa zote unatakiwa kutafakari neno la Mungu siyo kuwaza shida, taabu na masumbufu ya dunia hii. Kulitafakari Neno huja baada ya kulisoma, Daudi alisema: ”Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi“ (Zab. 119.11).
Alilisoma na kisha akalihifadhi moyoni. Neno hilo katika hazina ya moyoni, likawa mshauri, mwongozo na faraja wakati wa majaribu, mapito au mateso. Na kwa kulitamka likafanyika fimbo ya kumwangamiza adui, na kufungua milango ya baraka iliyofungwa na adui na pia likatumika hata kubadilisha mazingira kama Ezekia alivyotamka uhai kwa mifupa, ikainuka ikiwa hai na kuwa kikundi kikubwa cha watu.
MAFUNDISHO.
Ili uwe na maisha yenye mwelekeo wa ki-Mungu na ya mfano, epuka kabisa kuwaza mambo mapotofu, epuka mazungumzo mafu yasiyo na uhai wa ki-Mungu maana yatakuharibu wewe pamoja na wakusikilizao, pia matendo yoyote yaliyo kinyume na Neno la Mungu epukana nayo. Mungu alijua kuwa kijana huyu Yoshua asiposisitiziwa na Mungu mwenyewe, asipoishi kwa Neno ambalo ndiyo lishe bora ya roho yake, angeharibikiwa, na hapo kusudi la Mungu la ukombozi wa wana wa Israel lingeyumba. Hali kadhalika wewe usipoishi kwa kulitii Neno na kufanya kama linavyokuagiza, adui atayumbisha mpango wa Mungu katika maisha yako, matokeo yake ni kuchanganyikiwa, kukata tamaa na hata kufa kabisa kiroho. Lakini ukisimama pasipo kujali mazingira yanayokuzunguuka, Mungu anao mpango mzuri sana na maisha yako na ndiyo maana (amekuita). Yumkini wewe ndiye wa kwanza kumpa Yesu maisha yako katika familia au ukoo wako. Mungu anategemea kukutumia wewe kulifikisha kundi hilo nchi ya ahadi kama alivyomtumia Yoshua. Zoezi hilo litafanikiwa iwapo utakuwa hodari tu na mwenye ushujaa mwingi, na kutenda sawasawa na Neno kama linavyoletwa kwako na Roho Mtakatifu mwenyewe kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujumbe huu unaousoma sasa.


IMEANDALIWA NA
ABEL R. REGINALD
0713 900 905

Sunday, June 23, 2013

Matokeo ya mechi za leo tarehe 23/06/13(Paroko Cup)


Matokeo ya mechi ya Kundi A tarehe 23/06/2013



Kigango cha Damu Takatifu 5 Kigango cha Mt. Gasper 2



Matokeo ya mechi ya Kundi B tarehe 23/06/2013



Kigango cha Mt.Rafael Mbweni Malindi 2 Kigango cha Mt.Anthony wa Padua Mbweni Mpiji 0



MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI A
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint
Damu Takatifu Boko11005 2 3
Mt.Gasper Boko21 1045 3
Mbweni101002 0


MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint
RAFAEL110020 3
MARIA DEL MATHIAS100133 1
ANTHONY WA PADUA211135 1

Friday, June 21, 2013

MSALABA WA YESU

Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa mamlaka ya Ponsio Pilato labda tarehe 7 Aprili 30 BK.
Adhabu hiyo kali ilianza huko Uajemi na kuenea hadi Dola la Roma ambalo liliitumia hasa katika maeneo ya pembeni.
Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndio kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.
Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa, hasa uchoraji.
Na tunatakiwa kuyafananisha mahangaiko ya maisha yetu kama msalaba wa Yesu tukiwa na imani kuwa mwisho tutaufikisha na tutafariki na kurudi kwa Mungu Baba hapo tutapata raha ya milele pamoja na Watakatifu wote.

ziara ya Mbulu tarehe 26June13

Tumsifu Yesu Kristo,
YAH:SAFARI YA ZIARA YA UINJILISHAJI PAROKIA YA DAUDI JIMBO LA MBULU MKOANI MANYARA.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, siku ya jumatano tarehe 26/06/2013, VIWAWA wataanza safari ya kuelekea Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara.
Kwanza tunatoa shukrani kwa Wazazi, Walezi, Viongozi wa JNNK kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia kwa kuwachangia Vijana na kuwaruhusu kushiriki katika ziara hii.
Safari itaanzia Parokiani Boko saa kumi na moja asubuhi, na tunatarajia kwenda kupumzika katika mji wa Karatu Mkoani Arusha, Siku ya Alhamisi tarehe 27/06/13 tutaenda Ngorongoro na mchana tutafanya ziara katika Parokia ya Endabashi, Jioni tutaenda Parokia ya Mt. Francisco wa Asizi –Kijiji cha Daudi hapo tutakaa mpaka tarehe 29/06/2013. Jumapili Tarehe 30/06/2013 tutaenda Parokia ya Mt. Yosefu Mfanyakazi(JIMBONI), na kushiriki Ibada ya Misa Takatifu na baadaye kukutana na Vijana wenzetu. Jioni tutaanza safari na tutapumzika Karatu na tarehe 01/-7/2013, saa kumi na moja asubuhi tutaanza safari ya kurudi Dar es salaam.
Tuzidi kuombeana katika kufanikisha ziara hii ya kitume. Tunamwomba Mungu aongoze safari yetu, malaika mikaeli mlinzi wa safari atuongoze.
Mapendo..................................................

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR