Sunday, February 24, 2013

Jimbo Katoliki la Mbulu

Jimbo katoliki la Mbulu (kwa Kilatini Dioecesis Mbuluensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Arusha.
Askofu wake ni Beatus Kinyaiya.

Historia

  • 1943: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Mbulu kutokana na Apostolic Vicariate ya Dar-es-Salaam
  • 1952: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate ya Mbulu
  • 25 Machi 1953: Kufanywa dayosisi

Uongozi

  • Maaskofu wa Mbulu
    • Beatus Kinyaiya (since 2005)
    • Juda Thadaeus Ruwa’ichi OFMCap (1999 – 2005)
    • Nicodemus Atle Basili Hhando (1971 – 1997)
    • Patrick Winters SAC (1953 – 1971)
  • Vicar Apostolic wa Mbulu
    • Patrick Winters SAC (1952 – 1953)
  • Prefect Apostolic wa Mbulu
    • Patrick Winters SAC (1944 – 1952)

Takwimu

Eneo ni la kilometa mraba 16,057, ambapo kati ya wakazi 995,000 (2006) Wakatoliki ni 269,620 (27.1%).

MALENGO YA ZIARA YA MBULU

Lengo kubwa la ziara hii ni kwaona Vijana wenzetu na kushirikiana nao jinsi ya kueneza Injili  pia kujenga mashirikiano katika maswala ya kiuchumi na maendeleo kwa ujumla pia tutapata nafasi ya kujifunza tamaduni mpya kutoka katika makabila mbali mbali yalipo huko

Zaidi tutafika katika kanisa Kuu la Jimbo la Mbulu na kujionea ukubwa wake ambapo ndilo kanisa kubwa kuliko yote hapa Africa Mashariki.

mwisho tutaenda Mbuga ya wanyama ya Ngorongoro kuona uzuri wa nchi Yetu na Maajabu ya Mungu.

 KUWA TAYARI NA ANZA MAANDALIZI SASA KWA KUJAZA FORM NA KUWAKILISHA FEDHA YAKO NAFASI NI KWA VIJANA 60 TU.

Matangazo ya Juma la lijalo......

      JUMAMOSI TAREHE 02/03/2013
  1.  Kutakuwa na mafungo ya jubilee ya Miaka 200 ya Shirika la Damu Takatifu, Mafungo hayo yatafanyikia katika kituo cha Hija cha Shirika kilichopo Parokia ya Mt. Gasper De Bufalo Mbezi Beach na yataanza saa 2:00 asubuhi
  2. Kamati tendaji ya VIWAWA Kigango cha Mt. Rafael Mbweni Malindi watafanya kikao saa kumi na moja jioni Kigangoni...Pia Vijana wote wanakumbushwa kufika saa kumi Jioni kwa ajili ya Mazoezi ya Kwaya.
  

       JUMAPILI TAREHE 03/03/2013
      RATIBA ZA IBADA ZA MISA TAKATIFU
KIGANGO CHA BOKO.
MISA YA KWANZA 12:30-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI     SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MBWENI 
MISA YA KWANZA SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 4:00-5:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 2:00-4:00 ASUBUHI

Halmashauri ya VIWAWA Parokia watakuwa na Kikao mara baada ya Misa ya Pili Saa 4:00 asubuhi kikao kitafanyikia Parokiani Boko wajumbe wote mnatakiwa kufika Bila kukosa.

Wasilisha Mchango wako wa Hija ya Bagamoyo kwa Mhazini wa Jumuiya yako au Kigango chako Kabla ya Tarehe 09/03/2013

Thursday, February 21, 2013

Yesu Kristo

Yesu Kristo (kutoka Kigiriki Ιησους Χριστός (Iesus Christos) ni jina la kawaida kati ya Wakristo kumuitia Yesu wa Nazareti (Yesu Mnazareti).
Kwa asili ni tamko la imani lenye sehemu mbili: jina "Yesu" na cheo "Kristo".
Kristo ni tafsiri ya Kigiriki ya neno la Kiebrania- "mashiah" (Masiya).
Katika lugha ya Kigiriki "Yesu Kristo" mara nying`i ni sentensi kamili, maana yake "Yesu ndiye Masiya wa Mungu", yaani Yesu ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale na kutazamiwa na Israeli.
Katika aya nyingine za Agano Jipya "Yesu Kristo" tayari imetumika kama jina. (linganisha: rais Mkapa, au: Mkapa rais - si yule Mkapa mwingine...)

Yesu alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 B.K.). Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kwanzia ujio wake (ulivyokadiriwa kimakosa katika karne ya 6).

 

Mazingira yake

Nchi ambayo Yesu alizaliwa akafundisha ni nchi ileile ambayo Mungu aliwaahidia Waisraeli tangu zamani za Abrahamu, ni nchi ileile waliyoiteka chini ya Yoshua, ni nchi ileile waliyoirudia kutoka utumwani Babeli.
Lakini wakati wote wa Agano Jipya, yaani tangu Yesu alipozaliwa hadi mwisho wa maisha ya mitume wake, nchi hiyo haikuwa huru, bali chini ya himaya ya Warumi, ingawa pengine hao waliwakabidhi vibaraka, yaani watawala wenyeji waliowekwa na wakoloni.
Vibaraka hao ni Herode Mkuu (37 KK-4 KK) na wazawa wake, ambao tena hawakuwa Waisraeli halisi bali Waedomu ingawa kabila lao lililazimishwa kuingia dini ya Kiyahudi karne iliyotangulia. Ukoo huo unajulikana kwa ukatili, uchu wa madaraka na uzinifu wake.
Vilevile maliwali wa Kirumi waliowekwa pengine kutawala nchi au sehemu fulani walionyesha mara nyingi ukatili na dharau kwa Waisraeli na dini yao, hata kusababisha chuki na mapigano kati ya jeshi na wananchi. Mfano mmojawapo ni Ponsyo Pilato aliyesimamia Uyahudi kuanzia mwaka 26 hadi 36 B.K.
Mbali na hayo, utawala wa Roma, ulioenea Ulaya Magharibi na Kusini, Afrika Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati kupakana na Iraq ya leo, kwa jumla ulihakikisha hali ya amani kwa muda wote wa Agano Jipya na karne za kwanza za Kanisa. Hali hiyo, pamoja na umoja wa dola hilo lote, na urahisi wa mawasiliano kwa njia ya barabara zilizotengenezwa na Warumi, na uenezi wa lugha ya kimataifa (Kiyunani yaani Kigiriki cha zamani), ilichangia kasi ya uenezaji wa habari njema (Injili). Lugha hiyo ndiyo iliyotumiwa na waandishi wote wa Agano Jipya ili vitabu vyao viwafaidishe watu wengi zaidi, ingawa baadhi yao hawakuijua vizuri.
Lugha asili ya Yesu na ya Mitume ilikuwa Kiaramu ambacho ni jamii ya Kiyahudi na ambacho polepole kilishika nafasi yake kati ya Wayahudi kuanzia karne ya sita K.K. Hao wote walitokea mkoa wa Galilaya, uliokuwa na mchanganyiko wa watu (Waisraeli na mataifa), kiasi kwamba huko Wayahudi wenyewe walifuata kwa urahisi desturi za Kiyunani hata wakadharauliwa na wenzao wa Kusini (Yerusalemu na mkoa wa Yudea).
Kati ya mikoa hiyo miwili ulienea mkoa wa Samaria ambao wakazi wake walijenga uadui mkubwa na Wayahudi baada ya uhamisho wa Babeli, walipokataliwa kuchangia ujenzi wa hekalu la pili la Yerusalemu.

Maisha yake

Dionisi Mdogo, mmonaki aliyeanzisha (mwaka 533 hivi) mtindo wa kuhesabu miaka kuanzia kuzaliwa Yesu kurudi nyuma (K.K.) au kwenda mbele (B.K.), alikosea hesabu zake. Leo tunakisia Yesu alizaliwa mwaka 6 hivi K.K. kwa sababu alizaliwa Bethlehemu chini ya Herode Mkuu aliyefariki mwaka 4 K.K.
Huyo alipojaribu kumuua mtoto Yesu, familia takatifu ilikimbilia Misri mpaka baada ya kufa kwake. Hapo ikarudi Galilaya hata Yesu akajulikana kwa jina la kijiji cha Nazareti kilichodharauliwa na Wagalilaya pia. Ndipo alipokulia na kuishi akifanya kazi ya ufundi.
Mwaka 26 hivi B.K. ndugu yake Yohane Mbatizaji aliacha maisha ya jangwani na kuanza kuhubiri toba kandokando ya mto Yordani. Kwa kuwa Waisraeli walikosa manabii kwa muda mrefu, na walitamani sana ukombozi, walimuendea kwa wingi hata wakamtia hofu Herode Antipa.
Ingawa huyo akamfunga mapema akamuua, kazi ya Yohane ilikuwa imetimia kwa sababu aliweza kuwaandaa Waisraeli wengi (hasa watu wadogo na wakosefu) wampokee Yesu aliyebatizwa naye. Katika nafasi hiyo Yohane alimtambulisha kama Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu.
Ndipo Yesu naye alipoanza kuhubiri, lakini pia kutenda miujiza ya kila aina, akapata haraka wafuasi wengi. Kati yao akachagua Mitume wake 12 kama msingi mpya wa taifa la Mungu. Alifanya kazi hizo kuanzia Galilaya, akitangaza ujio wa ufalme wa Mungu, kwa maana ya kwamba ufalme uliotazamiwa na Wayahudi umewajia kwa njia yake.
Ingawa hakupitia shule yoyote ya Biblia, Yesu alionekana anafundisha vizuri kuliko walimu wa sheria wa kawaida, kama mtu mwenye mamlaka juu ya Torati. Mafundisho yake yalilingana na yale ya Mafarisayo kuliko na yale ya Masadukayo, lakini alishindana pia na hao wa kwanza.
Kijicho na upinzani vikazidi hasa Yerusalemu, walipoanza kufanya njama za kumuua. Ingawa Yesu alijua hayo, alijikaza kwenda katika mji mtakatifu autangazie habari njema na kufia huko. Baada ya kupokewa kwa shangwe kabla ya sherehe ya Pasaka ya mwaka 30 (au 33) akakamatwa na baraza la Israeli kwa tuhuma ya kufuru ya kujilinganisha na Mungu, halafu akakabidhiwa kwa liwali wa Kirumi aliyekuwa na mamlaka ya kutoa adhabu ya kifo. Baada ya kikao ambapo Wayahudi walitafuta kisingizio cha kisiasa, Ponsyo Pilato akalazimika kuagiza Yesu asulubiwe, na kisha kufa kwake kaburi lilindwe na askari.
Hata hivyo siku ya tatu kaburi likaonekana tupu, na Yesu akaanza kuwatokea wanafunzi wake wa kike na wa kiume kwa muda wa siku arubaini, halafu akapaa mbinguni mbele ya macho yao.
Habari hizo zikatangazwa kwa sauti tu kwa miaka kadhaa, halafu zikaanza kuandikwa. Kanisa linaheshimu kwa namna ya pekee, kama ushuhuda mkuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu na kama moyo wa Maandiko matakatifu yote, Injili nne zilizoandikwa na Marko, Mathayo, Mwinjili Luka na Yohane kati ya mwaka 65 na 100 hivi.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>inaendelea>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Msalaba wa Yesu

Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa mamlaka ya Ponsio Pilato labda tarehe 7 Aprili 30 BK.
Adhabu hiyo kali ilianza huko Uajemi na kuenea hadi Dola la Roma ambalo liliitumia hasa katika maeneo ya pembeni.
Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndio kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.
Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa, hasa uchoraji.
Na tunatakiwa kuyafananisha mahangaiko ya maisha yetu kama msalaba wa Yesu tukiwa na imani kuwa mwisho tutaufikisha na tutafariki na kurudi kwa Mungu Baba hapo tutapata raha ya milele pamoja na Watakatifu wote.

SAFARI YA NGORONGORO NA JIMBO LA MBULU

 Ule mchakato wa Ziara katika Jimbo la Mbulu na kutembelea Mbuga ya Ngorongoro umekamilika, sasa kazi ni kwako kijana kuanza kufanya Maandalizi ya Ushiriki wako..ni nafasi ya pekee sana kwetu...

Tarehe 26-30/06/13..Vijana wa Parokia ya Boko tutafanya ziara ya kuinjilishi katika Parokia ya Daudi iliyopo Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara......ikiwa ni pamoja na kutembelea Kanisa kuu la Jimbo la Mbulu ambalo ndilo kanisa Katoliki kubwa kuliko yote hapa Tanzania na la tatu kwa ukubwa Barani Afrika.
Pia tutatembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro na kujionea mengi

Kwa mchango wa Tshs 150,000/= tu wahi sasa kujiandikisha nafasi ni kwa vijana 60 tu........wasiliana na uongozi wa vijana mahali ulipo au waone viongozi wa Jumuiya yako.

Tuesday, January 22, 2013

nembo ya mwaka wa imani





Nembo ya Mwaka wa Imani
Imeundwa kwa alama mbalimbali zinazobeba maana maalum.
A) Mashua: Hii ni ishara ya Kanisa linalosafiri.
B) Mlingoti: Huu ni Msalaba ambao juu yake kuna monogramu (chapa ya herufi zaidi ya moja zinazochanganyika pamoja, moja juu ya nyingine) IHS. Hizi ni herufi tatu za kwanza za Kigriki za jina la Yesu: I = Iota, H = eta, S = Sigma. Alama hizi zinatumika pia kuonyesha kifupisho cha jina la Yesu ambapo kwa kilatini zinatumika kusimama badala ya maneno: Iesus Hominum Salvator; yaani, Yesu Mwokozi wa Wanadamu.
C) Mduara: Nyuma ya monogramu ipo alama ya mduara ambao unaizunguka pia monogramu hiyo. Hii ni alama ya Jua ambayo inawakilisha Ekaristi Takatifu.
(Tafsiri ya maelezo, TEC, 2012)
Nembo ya Ofisi ya Vijana
Vijana wane walioshikana mikono wanasimamia vyama vya Kitume vinavyounda umoja wa Vijana. Katikati kuna alama ya kamba, chini ya neno Fidei. Kamba ni chombo cha kufunga vitu viwili au zaidi. Kamba inayoshikanisha vijana wote ni Imani. Neno Fidei ni neno la Kilatini lenye maana, “ya Imani”. Yaani, umoja huu unahusu imani.
Programu zote za Mwaka wa Imani zitakuwa na nembo hii. Pia, kauli mbiu ya mwaka huu, kwetu vijana, itakuwa pia sala, maneno ya mwinjili Luka,


“Bwana, utuongezee imani

Luka 17:5.
                                   2012—2013

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR