Wednesday, February 27, 2013

HISTORIA FUPI YA MAKANISA YA MWANZO YA ZANZIBAR

WARENO 1500 – 1800

Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno.  Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya matumaini mema – Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao wa Afrika.
Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499 walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar.  Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la mwambao.  Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba.  Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman.  Jeshi hili la Oman inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.
Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi  kuwaka moto mji wa Mombasa, Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini, mbali na mafikio ya mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo za miongo za jahazi (waarabu). 

OASISI YA UVUMILIVU (OASIS OF TOLERANCE)

Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu.  Malezi yake katika maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa hivyi vyenye ustawi.  Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi katika bahari.  Alisimamia mipango  mikubwa ya upandaji miti, alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha mamia ya wageni.  Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi.  Na alijua kwamba biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa litaimarishwa kwa vitu na mambo mengine pamoja na usalama.  Vile vile alitarajia na kutambua kwamba angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za kibiashara zitakazo endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa hivyi.  Aliwakaribisha na kuwaomba wafanyabiashara kutoka India kufungua matawi ya ofisi zao ndani ya Zanzibar ili kuimarisha biashara.  Wafanyabishara hawa wengi kutoka India walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutekwa India na Uingereza.  Kwa maana hiyo, alianza kuwakaribisha maofisa wa kiingereza visiwani ili kuwakilisha maslahi ya raia hawa wahindi wa kiingereza.  Mara tu tena baadae alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na Serikali ya kiingereza na Serikali nyengine za Magharibi.
Majengo ya biashara yalijengwa ndani ya Mji Mkongwe na Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na Kiingereza.  Bandari ya Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia matengenezo Meli za kivita na vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara.  Meli hizi zilileta mapote ya ziada ya watu wa magharibi ndani ya Zanzibar.  Kama ni makaribisho mema ya wageni wengi katika Oasisi yake.  Sultani aliruhusu watu wa imani zote kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.
Akiwa Muislamu mwenye imani kamili, Sultani alionyesha mfano bora wa uvumilivu juu ya mahitajio  ya kidini ya watu wengine.  Wakati huo huo akijenga furaha na imani katika dini ya mababu zake, kwa bidii zote.  Warithi wake alifuata utaratibu wa Sultani Seyyid, wakiruhusu kuanzishwa mahekalu mengi tu ya kihindi, makanisa mawili, moja la kikatoliki na kiprostanti, sehemu za kimazishi za zoroastriani na misikiti kwa kila dhehebu kuu au dogo la kiislamu ndani ya mji mmoja.

1800 – 1900

WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)

Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa ndio waliobakia Zanzibar.  Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi.  Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini.  Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English Church Missionary Society).  Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi. 
Ukuwaji wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka 1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na wafanyakazi Afrika.  David Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara na ukiristo”.  Baadae Livingstone alitumia siku nyingi tu Zanzibar ambao alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu  kwa Afrika ya Kati (UMCA).  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham na Dublin.  Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi.  Kwa ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia   kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo yake.  Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea kufa kwa askofu.  Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa.  Askofu mpya, George Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu  liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika kati kati ya Afrika.  Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha Johanna,  maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano, upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar tarehe 31/08/1864.
Ujumbe huu ulipowasili ulipokewa na wamisionari wakatoliki wa Kifaransa.  Wamisionari wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya miaka minne kabla ya wamisionari wa kiingereza.  Katika mwezi Septemba mwaka 1860 Abbe Favat ambaye alikuwa Mfaransa mdini  maarufu mwenye nguvu alitiliana mkataba na Seyyid Said kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake katika Kisiwa cha Reunion na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake cha “mapadri wawili wasio watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa wakiishi katika makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo Shangani.  Jengo hili la watawa linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860, lakini ujenzi huu inawezekana ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla.  Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar kwa miaka 200.

Click here: Kuendelea ..........

Tuesday, February 26, 2013

Kwaresima ni kipindi cha toba, matendo ya huruma na utii kwa maagizo ya Mwenyezi Mungu

Wakati huu wa Kipindi cha Kwaresima sanjari na Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, kutubu na kumwongokea Mwenyezi Mungu, tayari kuanza hija ya maisha mapya, kwa kumtii Mwenyezi Mungu. Inafahamika kuwa, Imani bila matendo hiyo imekufa ndani mwake! Kumbe, kuna haja kwa waamini kumwilisha imani yao kwa Kristo na Kanisa lake kwa njia ya matendo ya huruma kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii, kila mtu akijitahidi kuwa kweli ni Msamaria mwema kwa jirani yake. Ni mwaliko wa kuwa na mwono mpana zaidi kwa kuwaangalia wote wanateseka kutokana na majanga asilia, vita na madhulumu.

Kwaresima kiwe ni kipindi cha maandalizi ya kina katika Maadhimisho ya Fumbo la Pasaka, yaani, mateso, kifo na ufufuko wa Kristo. Kwaresima iwawezeshe waamini kujenga fadhila ya imani, matumaini na mapendo katika Fumbo la Ufufuko wa Kristo, ili hatimaye, kuweza kulitolea ushuhuda.  Imani ya Wakristo wa mwanzo ilijikita katika Ufufuko, wakaliona Kaburi wazi, hapo ukawa ni mwanzo wa Habari Njema ya Wokovu inayojikita katika: maisha, maneno na matendo ya Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti.

DEKANIA YA MT.GASPER DE BUFALO-KUNDUCHI

Dekania ya Mt Gasper inazijumuisha parokia zilizipo 
Mbezi Beach, Kunduchi, Tegeta, Boko na Bunju.

Dekania Hii inajumla  ya Parokia  kumi mpaka sasa:

  1.  Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma -Mbezi Beach

  2. parokia ya Mt. Dominick - Mbezi Juu

  3. Parokia ya Mt. Gasper De Bufalo- Mbezi Chini(Machakani)

  4. Parokia ya MT. Agustino -Salasala

  5. Parokia Mt. Nicolous- Kunduchi

  6. Parokia ya Damu Takatifu-Tegeta

  7. Parokia ya Mt.Adrea Bahari Beach

  8. Parokia ya Madale

  9. Parokia ya Mwenye Heri Isidori Bakanja -Boko

  10. Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmel - Bunju

Ndani ya Dekania hii kuna Vituo vya Hija viwili(2)

Kituo cha Hija ya Vijana Jimbo la Dar es salaam- Parokia ya Boko

Kituo cha Hija ya Shirika la Damu Takatifu ya Yesu - Parokia ya Mt. Gasper- Mbezi Beach 

HISTORIA YA UJENZI WA KANISA LA MBULU

Shujaa wetu: Franz Wesinger-Mhandisi aliyejenga kanisa Katoliki Mbulu

  Kanisa la Mbulu ndilo kanisa kubwa kuliko yote Tanzania na la pili kwa ukubwa Afrika Mashariki kanisa hili lilijengwa na   Mhandisi Franz Wesinger aliyezaliwa mwaka 1928 huko Bavaria Ujerumani.
Mwaka 2003, akiwa na miaka 75 mhandisi Franz Wesinger ambaye pia ni msanifu wa majengo alirudi Tanzania kwa ajili ya kupanga ujenzi wa kanisa jipya la Katoliki Arusha na ni katika kipindi hicho ambacho mapadre wawili wa kanisa Katoliki jimbo la Mbulu walikumbwa na kashfa ya ufisadi kama baada ya kufuja jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni 340 kwa bei ya 1000 kubadili dola moja wakati huo  (dola 340,000). Mapadre hao, msaidizi wa askofu (Vicar General) John Nada na father Melkiadus Qameyu wa parokia ya Dareda walituhumiwa kupoteza kiasi hicho cha fedha baada ya kutapeliwa na mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Mohamed mrisho kuwa angeziongeza mara mbili....mafaza wakaingia mkenge...
Turudi kwa Franz Wesinger, huyu bwana alifanya mahojiano na gazeti la Arusha Times mwaka 2003 na haya ni sehemu ya maelezo yake kuhusu ujenzi wa Kanisa hilo
"Katika miaka 15 iliyopita, Jimbo la Mbulu limepiga hatua kubwa sana. Jitihada za awali za marehemu Askofu Hhando zimezaa matunda kwani walianza kidogo au kusema ukweli halisia walianza bila fedha lakini waliweka imani yao kwa Mungu huku wakitumia msaada kidogo kutoka kwa wamihionari kutoka Ulaya na ujenzi ulianza. Amini usiamini, walianza ujenzi wakitumia sepetu lililovunjika na toroli la mbao. Kanuni kuu ilikuwa kubana matumizi na kuhudumu (huduma) pamoja kukawa kichocheo kikubwa katika jimbo zima kumtumikia Mungu" alisema Franz
"Hata baada ya ujenzi na kanisa kuwekwa wakfu zilibaki kontena 12 zikiwa zimejaa vifaa vya ujenzi, mashine, magenerata, jukwaa kubwa, magari mawili na lifti (cranes) bila kutumika"
"Kuna tofauti kati kuhudumu kwa imani na kutumaini kupata faida pasipo kufanya kazi" aliongeza Franz akizungumzia ufisadi uliotokea Mwaka moja baada ya ujenzi wa kanisa hilo kukamilika.
"Hata wana wa Israeli walimsahau Mungu na kuabudu ndama wa dhahabu baada ya Mungu kuwatoa utumwani mwa Wamisri na kuwapitisha katika bahari ya Shamu"
"Waisraeli walikombolewa lakini walitaka kupata faida pasipo kufanya kazi, hauwezi kumtumikia Mungu kwa ulanguzi"
Franz Wesinger alieleza kuwa anajisikia fahari kubwa sana moja ya sehemu maskini zaidi Tanzania ina Kanisa kubwa zaidi na zuri zaidi nchini na kuona fahari kuwa imejenga hilo kanisa lenyewe kwa msaada pekee wa Mungu"
Chini ya usimamizi wa Franz Wesinger ujenzi wa kanisa hili ambalo leo ni fahari kubwa kwetu ulikamilika kwa ufanisi wa hali ya juu na kutimiza ndoto ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo Kuu la Mbulu Marehemu Hhando. Franz Wesinger anatoa funzo la uaminifu na kuacha "legacy" kwa vizazi vijavyo. Sina uhakika kama bado yupo hai lakini Franz Wesinger alifanya kazi kubwa sana tofauti na "wahandisi" wetu ambao ninauhakika kisingebaki kitu baada ya ujenzi na katu kazi ya ujenzi wa kanisa hilo usingekamilika.
 

MATANGAZO YA JUMA TAREHE 02-03/03/13

  JUMAMOSI TAREHE 02/03/2013
  1.  Kutakuwa na mafungo ya jubilee ya Miaka 200 ya Shirika la Damu Takatifu, Mafungo hayo yatafanyikia katika kituo cha Hija cha Shirika kilichopo Parokia ya Mt. Gasper De Bufalo Mbezi Beach na yataanza saa 2:00 asubuhi.
  2.  
  3. Kamati tendaji ya VIWAWA Kigango cha Mt. Rafael Mbweni Malindi watafanya kikao saa kumi na moja jioni Kigangoni...Pia Vijana wote wanakumbushwa kufika saa kumi Jioni kwa ajili ya Mazoezi ya Kwaya.


       JUMAPILI TAREHE 03/03/2013
      RATIBA ZA IBADA ZA MISA TAKATIFU
KIGANGO CHA BOKO.
MISA YA KWANZA 12:30-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI     SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MBWENI 
MISA YA KWANZA SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 4:00-5:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 2:00-4:00 ASUBUHI.

KIKAO CHA HALMASHAURI YA VIWAWA PAROKIA

Halmashauri ya VIWAWA Parokia watakuwa na Kikao mara baada ya Misa ya Pili Saa 4:00 asubuhi kikao kitafanyikia Parokiani Boko wajumbe wote mnatakiwa kufika Bila kukosa.

.....Wasilisha Mchango wako wa Hija ya Bagamoyo kwa Mhazini wa Jumuiya yako au Kigango chako Kabla ya Tarehe 09/03/2013..........

Monday, February 25, 2013

YA KWETU TENA 2013

Ule mchakato wa Ziara katika Jimbo la Mbulu na kutembelea Mbuga ya Ngorongoro umekamilika, sasa kazi ni kwako kijana kuanza kufanya Maandalizi ya Ushiriki wako..ni nafasi ya pekee sana kwetu...

Tarehe 26-30/06/13..Vijana wa Parokia ya Boko tutafanya ziara ya kuinjilishi katika Parokia ya Daudi iliyopo Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara......ikiwa ni pamoja na kutembelea Kanisa kuu la Jimbo la Mbulu ambalo ndilo kanisa Katoliki kubwa kuliko yote hapa Tanzania na la tatu kwa ukubwa Barani Afrika.
Pia tutatembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro na kujionea mengi
WANYAMA WAKIWA WAMEPUMZIKA KANDO YA ZIWA HUKO NGOROGORO  

Kwa mchango wa Tshs 150,000/= tu wahi sasa kujiandikisha nafasi ni kwa vijana 60 tu........wasiliana na uongozi wa vijana mahali ulipo au waone viongozi wa Jumuiya yako.

SOMO LA LEO FEB 25 JUMA LA 2 LA KWARESIMA


 S0M0 LA 1


“Ee Bwana, Mungu mkuu na
unayetisha, anayeshika agano lake
la
upendo kwao wanaompenda na kutii
maagizo yake, tumetenda dhambi na
5
kufanya mabaya. Tumekuwa waovu na
tumeasi, tumegeuka mbali na maagizo yako
na sheria zako.  Hatukuwasikiliza watumishi

wako manabii, ambao kwa jina lako
walisema na wafalme wetu, wakuu wetu,
baba zetu na watu wote wa nchi.
Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini
siku hii ya leo tumefunikwa na aibu,
wanaume wa Yuda na watu wa Yerusalemu
nayo Israeli yote, wote walio karibu na walio
mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa
sababu ya sisi kukosa uaminifu kwako. Ee
8
BWANA, sisi na wafalme wetu, wakuu wetu
na baba zetu tumefunikwa na aibu kwa
sababu tumefanya dhambi dhidi yako.
9
BWANA wetu ni mwenye rehema na
anayesamehe, hata ingawa tumefanya uasi
dhidi  yake,
10
hatukumtii BWANA Mungu
wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia
kwa watumishi wake manabii

INJILI YA LEO 

6
huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Kuwahukumu Wengine
37
“Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa.
Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni,
nanyi mtasamehewa.  Wapeni watu vitu, nanyi
38
mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na
kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu
watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa
kipimo kile kile mpimacho, ndicho
mtakachopimiwa. 
 TUTAFAKARI PAMOJA.......

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR