Thursday, February 12, 2015

Askofu mteule wa jimbo la Shinyanga amekiri Kanuni ya Imani na kula kiapo cha utii kwa Kanisa anapotekeleza dhamana na wajibu wake wa kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu,


Askofu mteule Liberatus Sangu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Jumanne tarehe 10 Februari 2015 katika Ibada ya Liturujia ya Neno la Mungu, iliyoongozwa na Askofu mkuu Savio Hon Tai-Fai, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu amekiri Kanuni ya Imani na kula kiapo cha utii kwa Kanisa anapotekeleza dhamana na wajibu wake wa kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu, huku akiwa ameungana na Maaskofu wenzake.

Alhamisi, 12 Februari 2014 Juma la 5 la Mwaka

"Asali itokayo Mwambani"

Mwa 2:18-25;
Zab 128:1-5;
Mk 7:24-30;

Imani huamisha milima

Katika Injili ya leo, Yesu anamfukuza pepo kutoka kwa binti wa mwanamke Mkanaani. Yesu, hapa, alijionyesha kama mwanga wa mataifa. Wayahudi walimkataa Kristo, lakini watu wa mataifa wali mkaribisha na wakamwamini. Mwanamke wa Kikanaani, alikuwa mgeni kwa jamii ya Israeli, lakini imani yake katika Yesu ilkua zaidi kuliko imani ya Wayahudi. Imani ya mwanamke huyu ilikuwa kubwa. Hata katika tusi dhahiri ya Yesu, ambaye alimwita 'mbwa,' yeye aliibuka kama mwanamke wa imani kubwa, ambayo haiwezi kulinganishwa na yoyote ya Wayahudi. Hii ilikuwa kama ile ya kumpima Ibrahimu. Je, una imani kama mwanamke wa Kikanaani?

Maombi: Bwana, Nisaidie kuongeza Imani yangu kwako Amina!

Bonyeza LIKE kwa ukurasa wetu
www.facebook.com/viwawaboko

tarehe 18/02/2015, ni jumatano ya majivu tuanze kujianda kwa safari ya ukombozi........

Sunday, February 8, 2015

Masomo ya dominika ya 5 mwaka B wa kanisa(tarehe 08/02/2015


08

 FEBRUARY
 Jumapili: Dominika ya 5 ya Mwaka "B".
SOMO  1. Ayu. 7:1-4,6-7
 Ayubu alianza kusema:Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je!si kama siku za mwajiri? Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, kama mwajiri anayetazamia mshahara wake; ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha. Hapo nilalapo chini,nasema, nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, nazo zapita pasipokuwa na matumaini. kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; jicho langu halitaona mema tena.

Monday, February 2, 2015

Mwaka watawa wafunguliwa rasmi Jimbo kuu la Dar es salam

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linafungua rasmi Maadhimisho ya Mwaka wa Watawa Duniani, uliotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 2 Februari 2015, Siku kuu ya kutolewa Bwana Hekaluni, sanjari na maadhimisho ya siku ya kumi na tisa ya watawa duniani, iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Maadhimisho haya yanafanyika katika ngazi ya Kijimbo na katika baadhi ya Majimbo makuu.  
Hayo yamesemwa na Askofu Renatus Nkwande, Mwenyekiti wa Tume ya Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican. Kwa namna ya pekee anasema, Watawa wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa imani dhidi ya ukanimungu, kwa kujikita katika maongozi ya Mungu, Injili ya Kristo na Mashauri ya Kiinjili.

Mons. Liberatus Sangu ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania!

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Liberatus Sangu kutoka Jimbo Katoliki la Sumbawanga, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Askofu mteule Sangu alikuwa ni Afisa mwandamizi katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini Vatican.

Sunday, February 1, 2015

Tafakari ya Jumapili ya 4 ya Masomo ya Mwaka B tarehe 01/02/2015

Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza
anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya kale kwamba atamtuma Nabii atakayetangaza hukumu zake kwa haki, atakayesema yale ya Bwana na kama atasema kinyume atakufa. Manabii wengi walitangaza ujumbe wa Mungu lakini hasa katika zama zetu Mungu anasema nasi kwa njia ya Masiha kama ambavyo Wayahudi walielewa ujumbe huo wa Neno la Mungu.

Masomo ya Tarehe 01/02/2015, Jumapili: Dominika ya 4 ya Mwaka "B".

01

February

 Jumapili: Dominika ya 4 ya Mwaka "B".
SOMO  1. Kumb. 18:15-20

 Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huo mkubwa, nisije nikafa. Bwana akaniambia, wametenda vyema kusema walivyosema . Mimi nitawaondoshea Nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Lakini Nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR