Saturday, February 21, 2015

Masomo ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima Mwaka 'B' wa Kanisa 2015

21

 FEBRUARY
 Jumapili ya 1 ya Kwaresima Masomo ya Mwaka "B".
SOMO  1: Mwa. 9:8 - 15

Somo katika kitabu cha Mwanzo.
Mungu akamwambia Nuhu, na wanae pamoja naye, akisema, mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi, tena na uzao wenu baada yenu; tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi; ndege na mnyama wa kufungwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi. Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika, wala hakutakuwa tena gharika,baada ya hayo, kuiharibu nchi. Mungu akasema, hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.

WIMBO WA KATIKATI. Zab. 25:4-9, (k) 10. 
K. Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli, kwao walishikao agano lake na shuhuda zake..

Thursday, February 19, 2015

Makala ya Rais Kikwete juu ya Uzinduzi wa Sera Mpya ya Elimu Tanzania ul...

Masomo ya Alhamisi ya Majivu Mwaka B wa kanisa Tarehe 19/02/2015

19

 FEBRUARY
 Kipindi cha Kwaresima: Alhamisi ya Majivu. Mwaka "B".
SOMO  1: Kumb. 30:15 - 20

Musa aliwaambia watu akisema: Angalia, nimekuweka leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; kwa hivi nikuagiziayo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zae upate kuwa hai na kuongezaka; Bwana Mungu wako apate kukubarikia katka nchi uingiayo kuimiliki. Lakini moyo wako ukigeuka, usipotaka kusikiza, laini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia; nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia, hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukayo Yordani, uingie kuimiliki. Zasishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako kuitii sauti yake, na kushikamana naye, kwani hivyo ndivyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi ya Bwana aliyowaapia baba zako. Ibrahimu na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.

WIMBO WA KATIKATI. Zab. 1:1-4, 6. 
K. Heri mtu aiyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.

Wednesday, February 18, 2015

Masomo ya Jumatano ya Majivu

18

 FEBRUARY
 Kipindi cha Kwaresima: Jumatano ya Majivu. Mwaka "B".
SOMO  1: Yoe. 2:12 - 18

 Somo katika kitabu Cha Nabii Yoel
Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia , na kwa kuomboleza; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye haghairi mabaya. N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke, chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.
 Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, hata mataifa watawale juu yako; kwani wasema kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
 Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake. 

WIMBO WA KATIKATI. Zab. 51:1-4, 10-12, 15. 
K. Utuhurumie, ee Bwana kwa kuwa tumetenda dhambi 

Tuesday, February 17, 2015

Jumatano ya Majivu (ASH WEDNESDAY)

Jumatano ya Majivu ni siku ya kwanza ya kwaresima.
Jumatano ya Majivu Waamini hupakwa Majivu kichwani pamoja na kutamkiwa maneno ya kuhimizwa kufanya toba “ulitoka mavumbini na mavumbini utarejea.
Kwa kawaida siku hii ndiyo Kipindi cha kwaresima huanza rasmi . Waamini hufunga, mfungo unaofuata kilelezo cha Yesu kufunga siku Arobaini jagwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuunza utume wake mwenyewe

UMUHIMU WA JUMATANO YA MAJIVU.
Ili kuelewa vizuri maana na umuhimu wa kipindi hiki, tutazame kwa ufupi haya yafuatayo: 

RATIBA YA IBADA YA Jumatano ya Majivu

Vigango vyote vya Parokia ya Boko ibada itaanza saa 11:00 Jioni

Monday, February 16, 2015

Wasifu wa Padre Prosper Balthazar Lyimo aliyeteuliwa kuwa Askofu msaidizi, Jimbo kuu la Arusha, Tanzania

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Prosper Balthazar Lyimo, kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Arusha, Tanzania.
Wasifu wake
Askofu mteule Prosper Balthazar Lyimo alizaliwa Kyou – Kilema, Jimbo Katoliki la Moshi, tarehe 20 Agosti 1964 . Baada ya masomo yake ya shule ya msingi huko Maua na Arusha, alijiunga na Seminari ndogo ya Jimbo Katoliki Arusha. Alipata masomo yake ya Falsafa kwenye Seminari kuu ya Kibosho, iliyoko Jimbo Katoliki la Moshi na masomo ya Taalimungu alipata Seminari kuu ya Kipalapala, iliyoko Jimbo kuu la Tabora.
Baada ya majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa Jimbo kuu la Arusha kunako tarehe 4 Julai 1997. Tangu wakati huo amekuwa ni mlezi katika Seminari ndogo ya Jimbo kuu la Arusha kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 1999. Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2004 alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo kuu la Arusha. Kunako mwaka 2004 hadi mwaka 2007 alipelekwa na Jimbo kwa ajili ya masomo ya juu mjini Roma, kwenye Chuo kikuu cha Kipapa cha Urbaniana. Kunako mwaka 2007 hadi mwaka 2008 alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo kuu la Arusha
Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2011 Askofu mteule Prosper Balthazar Lyimo, alitumwa na Jimbo kuu la Arusha kwa ajili ya masomo ya juu nchini Canada na huko akajipatia shahada ya uzamivu kutoka katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Paul, kilichoko mjini Ottawa. Na kunako mwaka 2011 alirejea nchini Tanzania na kupangiwa kazi ya kuwa Katibu mkuu na Mkuu wa Mahakama ya Jimbo kuu la Arusha.
Askofu mteule Lyimo kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Mahakama ya Kanisa Jimbo kuu la Arusha.


NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR