Friday, June 21, 2013

MSALABA WA YESU

Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa mamlaka ya Ponsio Pilato labda tarehe 7 Aprili 30 BK.
Adhabu hiyo kali ilianza huko Uajemi na kuenea hadi Dola la Roma ambalo liliitumia hasa katika maeneo ya pembeni.
Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndio kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.
Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa, hasa uchoraji.
Na tunatakiwa kuyafananisha mahangaiko ya maisha yetu kama msalaba wa Yesu tukiwa na imani kuwa mwisho tutaufikisha na tutafariki na kurudi kwa Mungu Baba hapo tutapata raha ya milele pamoja na Watakatifu wote.

ziara ya Mbulu tarehe 26June13

Tumsifu Yesu Kristo,
YAH:SAFARI YA ZIARA YA UINJILISHAJI PAROKIA YA DAUDI JIMBO LA MBULU MKOANI MANYARA.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, siku ya jumatano tarehe 26/06/2013, VIWAWA wataanza safari ya kuelekea Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara.
Kwanza tunatoa shukrani kwa Wazazi, Walezi, Viongozi wa JNNK kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia kwa kuwachangia Vijana na kuwaruhusu kushiriki katika ziara hii.
Safari itaanzia Parokiani Boko saa kumi na moja asubuhi, na tunatarajia kwenda kupumzika katika mji wa Karatu Mkoani Arusha, Siku ya Alhamisi tarehe 27/06/13 tutaenda Ngorongoro na mchana tutafanya ziara katika Parokia ya Endabashi, Jioni tutaenda Parokia ya Mt. Francisco wa Asizi –Kijiji cha Daudi hapo tutakaa mpaka tarehe 29/06/2013. Jumapili Tarehe 30/06/2013 tutaenda Parokia ya Mt. Yosefu Mfanyakazi(JIMBONI), na kushiriki Ibada ya Misa Takatifu na baadaye kukutana na Vijana wenzetu. Jioni tutaanza safari na tutapumzika Karatu na tarehe 01/-7/2013, saa kumi na moja asubuhi tutaanza safari ya kurudi Dar es salaam.
Tuzidi kuombeana katika kufanikisha ziara hii ya kitume. Tunamwomba Mungu aongoze safari yetu, malaika mikaeli mlinzi wa safari atuongoze.
Mapendo..................................................

MSIMAMO WA LIGI YA PAROKO CUP LEO



Matokeo ya mechi ya Kundi A tarehe 21/06/2013




Kigango cha Mbweni 0 Kigango cha Mt. Gasper 2




Matokeo ya mechi ya Kundi B tarehe 19/06/2013




Kigango cha Mt anthony wa Padua Mbweni Mpiji 3 Kigango cha Mt.Maria del Mathias 3





MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013





PAROKO CUP 13 :KUNDI A
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint

Mt.Gasper Boko11002 0 3
Mbweni10 1002 0
Damu Takatifu Boko000000 0


MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013





PAROKO CUP 13 :KUNDI
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magoliwaliofungwapoint

ANTHONY WA PADUA100133 1
MARIA DEL MATHIAS100133 1
RAFAEL000000 0

Tuesday, June 18, 2013

Papa atoa wito: Semeni ndiyo kwa maisha na hapana kwa Kifo


Papa Fransisko ametoa wito kwa watu wote kuyatetea maisha na hapana kwa kifo. Kusema ndiyo kwa maisha na kukataa kila kitendo kinachotaka kukatisha uhai , kusema hapa kubwa kwa kifo. Papa alitoa wito huu wakati wa hotuba yake siku ya Jumapili asubuhi, ambamo Mama Kanisa aliadhimisha SIKu ya Injili ya Maisha “ Evangelium Vitae” .

Katika homili yake aliyoitoa mbele ya umati wa watu wapatao 200,000 waliofurika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , kuhudhuria Ibada ya Misa iliyoongozwa na Papa, na pia kwa ajili ya sala Ya Malaika wa Bwana, ibada na sala zilizofanyika katika mtazamo wa maadhimisho Mwaka wa Imani, siku ililega zaidi majitoleo ya Injili ya Maisha.

Katika homilia yake , Papa Francis, alitafakari Maandiko Matakatifu yanavyotuambia mara kwa mara, jinsi Mungu Mmoja Hai, ndiye mwenye kutoa maisha.

Hata hivyo, alisema kwamba "mara nyingi, watu hawachagui maisha, hawaikubali Injili ya Maisha bali hujiachia wenyewe kuongozwa na itikadi na njia yapotofu katika kufikiri, zenye kuwekea maisha kibambaza, njia zisizo heshimu maisha, kwa sababu wamekubali kuongozwa na nguvu za ubinafsi katika utafutaji wa maslahi faida, mamlaka na kujijifurahisha , na si kwa ajili ya upendo kwa wengine , au kujali manufaa ya wengine.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa, watu wana ndoto za kujenga upya "Mnara wa Babeli", mji wa mtu asiyekuwa na Mungu. Wanaamini kwamba kumkataa Mungu, kuukataa ujumbe wa Kristo na Injili ya Maisha, huwaongoza kwa namna fulani katika furaha, kuwa na uhuru kamili wa kutimiza malengo yao ya kibinadamu. Na kama Kama matokeo yake , Papa aliendelea, Mungu aliye hai huondolewa na badala yake huwekwa miungu mbadala mfululizo ya kibinadamu ambayo hulewesha mtu katika uhuru bandia , ambao mwisho wake hujenga aina mpya za mfumo wa utumwa na kifo.

Papa alimalizia homilia yake na wito kwa waamini, kuyaonamadhara hayo ni hivyo waseme Ndiyo kwa Mungu ambaye ni Upendo. Ndiyo kwa Maisha ya kushikamana na Mungu ndiye uhuru wa kweli na hamfadhaishi mtu.
Mara baada ya Ibada ya misa Takatifu, Papa aliongoza sala ya Malaika wa Bwana. Katika hotuba yake fupi, Papa alielekeza mawazo yake katika mifano ya watu walioyatetea maisha kikamilifu, akiangalisha katika tukio la Siku ya Jumamosi ambamo Mama Kanisa alimtagaza kuwa Mwenye Heri , baba wa watoto saba wa Capri Italy, aliyeuawa katika kambi za msongamano za Nazi mwaka 1944, ambaye aliyaokoa maisha mengi katika kambi hiyo , kabla ya kupoteza yake mwenyewe.

Papa pia aliitumia nafasi hiyo kusalimia washiriki wa Mkutano wa hadhara wa wanachama wa Harley-Davidson, kwa ajili ya kutumia kwa miaka 110, tangu kutengenezwa kwa pikipiki, yenye nembo hiyo ya Harley Davidson, ambayo inajulikana kuwa aina ya kipekee na mashuhuri Marekani. Kwa ajili ya sherehe hii zaidi ya wapanda pikipiki 100,000, walikusanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki hii. Kati yao 1400 wakiwa na pikipiki zao , walibarikiwa na Papa wakati huo wa sala ya Malaika wa Bwana.




MSIMAMO WA LIGI YA PAROKO CUP

Zikiwa zimepita siku mbili tangu ligi Ya paroko cup ianza, timu zimekuwa zikijiandaa kwa nguvu sana hivyo kufanya mashindano yazidi kuwa na joto, huku kila mmoja akitamba kuwa bigwa kwa mwaka huu.

kesho kuna mechi moja tu ya kundi B kati ya ANTHONY WA PADUA VS MARIA DEL MATHIS MECH ITAFANYIKA MBWENI MPIGI KUANZIA SAA KUMI JIONI na Ijumaa kutakuwa na mechi ya Marudiano kati ya Mbweni vs St. Gasper katika uwanja wa rafael

MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI A
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magolimagoli waliofungwapoint
MBWENI000000 0
DAMU TAKATIFU001000 0
RAFAEL000000 0


MSIMAMO WA LIGI YA Paroko cup 2013


PAROKO CUP 13 :KUNDI
TIMUMechiImeshindaImefungwaSare Magolimagoli waliofungwapoint
ANTHONY WA PADUA1
001
3
3
1
MARIA DEL MATHIAS1
00
03
3
1
RAFAEL000000 0

Saturday, June 15, 2013

MATANGAZO YA DOMINIKA TAREHE 16/06/13



  JUMAPILI TAREHE 16/06/2013
      RATIBA ZA IBADA 
KIGANGO CHA MH. ISIDORI BAKANJA- BOKO.
MISA YA KWANZA 12:30-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI     SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. FRANCIS WA ASIZ-MBWENI 
MISA YA KWANZA SAA 1:10-3:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 3:00-4:30 ASUBUHI

KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 1:00-3:00 ASUBUHI.
MISA YA PILI SAA 3:00-5:00

KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA-MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00-5:00.


MIKUTANO
kutakuwa na kikao cha halmashauri ya Walei Parokia ya Boko kuanzia saa 4:00 asubuhi, wajumbe wa kikao hichi ni viongozi wote wa vigango, Mwenyeviti wote wa vyama vya kitume na Kamati tendaji.

MATANGAZO
  1.  Vijana wote mnaoenda Mbulu mnatakiwa kukutana Parokiani boko saa 4:00 asubuhi ukumbi wa chekechea.
  2. Waamini wote unakaribishwa kwenye uzinduzi wa Paroko cup kesho saa nane mchana Parokiani Boko
  3. tunatarajia kufanya sherehe ya kuwapongeza mashemasi wetu Paul, Victor na Pascal kwa kupata daraja la upadre sherehe hizo zitafanyika parokiani bunju tarehe 08/07/2013 kila mshiriki anatakiwa kuchangia Tshs 5000 kwa ajili ya chakula na vinywaji.
  4. Maandalizi ya Tamasha la Vijana kwa mwaka 2013 yameanza na kila kijana anatakiwa kulipa tshs 7000 mwisho wa kuwakilisha mchango ni tarehe 02/08/2013 unawaza kufanya malipo kwa njia ya benk kwa jina na number hii :viwawa parokia ya boko account no 01524526820100 crdb bank tegeta branch
  5.  
  6.  
  7. tunawakumbusha vijana wote kuendelea kulipa ada kwa maendeleo ya chama chetu..... mapendo sana

Thursday, June 6, 2013

Picture za Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya VIWAWA Parokia ya Boko

 viongozi wakiwa katika semina fupi ya uongozi


 Masista walezi genny na Sabina wakisikiliza kwa makini kabisa
 Mkufunzi wetu Sista Catherine Oiso akitoa semina uongozi kwa halmashauri ya Viwawa boko
 Mkufunzi akiendelea kushoto ni Mhazini wa Parokia Happy mwikola na Katibu wa parokia Timoth Japhet
 uchovu wa semina na umakini wa viongozi hodari wenye hari ya kuongoza
 mhazini wa Parokia ya Bunju akiwa anafuatilia sisi bado ni ndugu na tunategemeana na kushirikiana







 Semina imeisha sasa Mwenyekiti wa Parokia  Ndugu Abel Reginald anafungua mkutano mkuu wa nusu mwaka
 katibu wa Parokia akisoma ripot ya chama kwa kipindi cha nusu mwaka
 Halmashauri ya VIWAWA Kigango cha Boko wakiwa na Sista Genny
 Halmashauri ya VIWAWA Kigango cha Mt. Raphael wakiwa na Masista walezi
 Halmashauri ya VIWAWA Kigango cha Mbweni wakiwa na Masista walezi
 Halmashauri ya VIWAWA Parokia ya Boko:kutoka kulia aliyesimama ni mwenyekiti wa Kigango cha mbweni Fabian Masanja, wa pili kutoka kushoto aliyesimama ni Mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rafael Annastela Ishebabi na watatu kutoka kushoto aliyekaa ni Mwenyekiti wa Kigango cha Boko Dickson

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR